Wednesday , 29 March 2023
Home Kitengo Maisha Elimu CBE yaja na klabu za ujasiriamali mashuleni
ElimuHabari

CBE yaja na klabu za ujasiriamali mashuleni

Spread the love

CHUO cha Elimu ya Biashara (CBE), kimepanga kuanzisha vilabu vya ujasiriamali kwa shule za sekondari mkoani Dar es Salaam na kwa kuanzia kimezindua klabu kama hiyo katika shule ya sekondari Temeke.

Chuo hicho kimesema vilabu hivyo vinalenga kuwawezesha wanafunzi kukua wakifahamu masuala mbalimbali ya biashara tangu utotoni ili waweze kuwa wajasiriamali siku za mbele.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa klabu hiyo kwenye shule ya sekondari Temeke jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Shahada za Juu, Tafiti na Ushauri wa chuo hicho, Dk. Tumaini Ubadius, alisema wanalenga kuzifikia shule zote za Dar es Salaam.

Dk. Tumaini alisema chuo hicho kimeona ni muhimu wanafunzi wakaanza kufundishwa kuhusu ujasiriamali wakiwa wadogo ili wanapohitimu elimu ya juu wawe na uelewa mpana kuhusu masuala ya biashara.

Mmoja wa wanafunzi wa shule ya sekondari Temeke akigawa vipeperushi vinavyozungumzia Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), wakati wa uzinduzi wa klabu ya ujasiriamali kwenye shule ya sekondari Temeke jijini Dar es Salaam leo.

Alisema kupitia mpango huo, chuo kitakuwa kikipeleka walimu wake kila siku ya Alhamisi kwaajili ya kufundisha wanafunzi wanaosomea mchepuo wa biashara masuala ya ujasiriamali.

“Tunataka kupunguza tatizo la watu kutafuta ajira ili wanapomaliza masomo yao waweze kujiajiri na tunachofanya ni kukuza vipaji na ubunifu walionao tangu wakiwa wadogo,” alisema

“Tumeona tuanze kuwajengea uelewa kuanzia huku chini ili kijana anapokuwa awze kuwa na ufahamu mazingira yanayomzunguka na changamoto zinazomzunguka kuwa fursa kwake kwa kusaidia jamii na kujiingizia kipato,” alisema

Alisema wamepanga kutembelea shule zote za Dar es Salaam na kuanzisha klabu kama hizo lakini wataenda kwenye mikoa ambayo CBE ina kampasi zake kama Mbeya, Mwanza, Dodoma na Zanzibar.

Mkuu wa shule hiyo, Ingia Mtenga alikishukuru chuo hicho kwa kuichagua shule hiyo kuwa ya kwanza kuanzisha klabu ya ujasiriamali na aliahidi kuwa wataitumia fursa hiyo vyema.

Mwanafunzi wa kidato cha tatu shule ya sekondari Temeke jijini Dar es Salaam, Faudhia Hamis, akionyesha umahiri wa kucheza na nyoka wakati Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), kilipoenda kuzindua klabu ya ujasiriamali shuleni hapo leo

Alisema shule hiyo ilianzishwa mwaka 2005 kwa kidatio cha kwanza hadi cha nne na kwa sasa inawanafunzi 2,526 na wanafunzi zaidi ya 500 wanasoma mchepuo wa biashara shuleni hapo.

“Kwa hiyo wazo lenu la kuanzisha klabu ya ujasiriamali hapa limekuja wakati mwafaka kabisa kwasababu wanafunzi wenhi wanasoma masomo ya biashara. Tunashukuru fursa hii kwa sababu ujasiriamali utaisaidia wanafunzi wetu kutatua changamoto zinazowazunguka,” alisema

“Kupitia klabu hii miongoni mwao tutapata wapishi wazuri wanaotengeneza keki, wasusi wazuri, watengeneza bustani wafuga kuku na watazitumia changamoto zilizoko kwenye jamii kuwaingizia kipato cha kuwawezesha kujitegemea na kusaidia wengine,” alisema

Aliwataka wanafunzi hao kusoma kwa bidii ili wafaulu na kupata nafasi za kwenda kusoma kwenye vyuo kama CBE ambako watapata elimu ya juu kuhusu ujasiriamali na biashara kwa ujumla.

“Tunaomba mafunzo mtakayotoa kupitia klabu hii yawe endelevu na ikiwapendeza naomba hawa watakaopata mafunzo ya ujasiriamali wapate mitaji midogo midogo ili waweze kuanzisha biashara ndogo ndogo ambazo zitawasaidia kujiingizia kipato,” alisema

Mkurugenzi wa Shahada za Juu, Tafiti na Ushauri wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), Dk. Tumaini Ubadius, akimpongeza mmoja wa wanafunzi wa chuo hicho kwa kipaji cha kucheza miziki ya bongo fleva wakati wa uzinduzi wa klabu ya ujasiriamali shuleni hapo leo.

Joshua Ibrahim anayesoma kidato cha tatu alipongeza hatua hiyo akisema kuwa itakuwa nan msaada mkubwa kwa wanafunzi kuwa na uelewa kuhusu biashara wakiwa shuleni.

“Tunashukuru kwa kuichagua shule yetu kuwa ya kwanza na itatusaidia kufahamu masuala ya biashara mapema kwa hiyo siku za baadaye hata mtu akienda chuo kikuu anakuwa na msingi mzuri alioupata sekondari,” alisema Joshua.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

ElimuHabari

Serikali yataka vijana  wajiunge na program atamizi ya biashara CBE

Spread the love  SERIKALI imewahamasisha vijana kujiunga na program atamizi inayotolewa na...

AfyaHabari

Ugonjwa wa ajabu ulioua watano Bukoka ni Marburg

Spread the loveWAZIRI wa Afya, Ummy Mwalimu amesema ugonjwa wa ajabu uliosababisha...

Elimu

Mfuko wa Jimbo Musoma Vijijini wamwaga mamilioni ujenzi maabara za sekondari

Spread the love  MFUKO wa Jimbo la Musoma Vijijini, Mkoa wa Mara,...

AfyaHabariHabari

Ugonjwa wa ajabu wadaiwa kuua watano Kagera, Serikali yatoa tahadhari

Spread the loveJUMLA ya watu watano wanaidaiwa kufariki dunia  katika vijiji vya...

error: Content is protected !!