Tuesday , 21 March 2023
Home Kitengo Maisha Elimu CBE yaanzisha Shahada 10 za Uzamili, CBE yajivunia wahitimu wanaoajirika
ElimuHabari

CBE yaanzisha Shahada 10 za Uzamili, CBE yajivunia wahitimu wanaoajirika

Kaimu Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara, (CBE), Prof Edda Lwoga, akizungumza wakati wa mkutano na maofisa watendaji wakuu wa mashirika na taasisi za fedha ulioandaliwa na chuo hicho kwaajili ya kufahamiana na kutoa maoni yao namna ya kuboresha chuo hicho.
Spread the love

CHUO cha Elimu ya Biashara (CBE), kimewataka wenye  kampuni na taasisi mbalimbali kupeleka wafanyakazi wake kupata mafunzo yatakayowawezesha kuboresha ujuzi wao sehemu za kazi.

Hayo yalisemwa leo jijini Dar es Salaam na Kaimu Mkuu wa Chuo hicho,  Prof Edda Lwoga, akizungumza wakati wa mkutano na maofisa watendaji wakuu wa mashirika na taasisi za fedha ulioandaliwa na chuo hicho kwaajili ya kufahamiana na kutoa maoni yao namna ya kuboresha chuo hicho.

Alisema chuo hicho kina uzoefu mkubwa wa kufanyakazi na sekta ya umma na sekta binafsi hivyo aliwahimiza kuwapeleka CBE kujifunza ili wapate ujuzi mbalimbali.

Alisema CBE ni chuo kikongwe kilichoanza mwaka 1965 na kilizinduliwa na Baba wa Taifa Hayati Mwalim Julius Nyerere na mwaka 1983 walianzisha Kampasi yao mkoani Mwanza.

Washiriki wa Mkutano wa Maofisa Watendaji Wakuu (CEOs) wakifuatilia mada zilizokuwa zikitolewa kwenye mkutano ulioandaliwa na Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), jana jijini Dar es Salaam kwaajili ya kubadilishana mawazo kuhusu kozi zinazotolewa na chuo hicho.

Alisema CBE imeendelea kutanuka kwa kuanzisha kampasi mbalimbali kwenye mikoa ya Dodoma na Mbeya na kwamba idadi ya wanafunzi wanaodahiliwa nayo imekuwa ikiongezeka mwaka hadi mwaka.

Alisema mbali na CBE kuwa chuo cha kwanza kutoa elimu ya biashara nchini kimeendelea kutoa kozi adimu na kwasasa wanatoa pia kozi ya utalii ili kuunga mkono jitihada za serikali za kutangaza vivutio vya utalii nchini.

Alisema serikali imewekeza sana kwenye miundombinu ya elimu hivyo na chuo hicho kimejitahidi kuwekeza kwenye kutoa mafunzo ya vitendo yanayomwezesha mwanafunzi kujiajiri au kuajiriwa anapomaliza masomo.

Baadhi ya washiriki wa mkutano wa asubuhi ulioandaliwa na Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), kwaajili ya maofisa watendaji wakuu wa mashirika na taasisi za fedha kwaajili ya kupata maoni yao kuhusu namna ya kuboresha kozi zinazotolewa na chuo hicho. Katikati ni Mkuu wa chuo hicho mstaafu, Profesa Emmanuel Mjema.

“Tunatoa elimu ambayo inalenga kuibua mawazo ya biashara miongoni mwa wanafunzi wetuhali ambayo imewawezesha wengi wakimaliza chuo wajiajiri na waajiri wengine,” alisema

Alisema katia kujitanua zaidi CBE imeanza kufundisha shahada 10 za Uzamili kwenye kampasi zake za Dar es Salaam na Dodoma, Shahada ambazo zimejikita kwenye maeneo ya biashara, rasilimali watu na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA).

Washiriki wa mkutano ulioandaliwa na Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), kwa maofisa watendaji wakuu wa mashirika na taasisi za fedha kwaajili ya kupata maoni yao kuhusu namna ya kuboresha kozi zinazotolewa na chuo hicho.

Aliwaomba wakuu hao wa kampuni na taasisi kupeleka wafanyakazi wao kwenye chuo hicho ili wawajengee uwezo wa kusaidia kukuza makampuni yao.

Alisema wanakozi mbalimbali ikiwemo ya ubora wa viwango, vipimo na mizani inayotolewa Dar es Salaam na kampasi ya Dodoma hivyo aliwataka wenye kampuni kuwapeleka wafanyakazi wao.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Elimu

Mfuko wa Jimbo Musoma Vijijini wamwaga mamilioni ujenzi maabara za sekondari

Spread the love  MFUKO wa Jimbo la Musoma Vijijini, Mkoa wa Mara,...

AfyaHabariHabari

Ugonjwa wa ajabu wadaiwa kuua watano Kagera, Serikali yatoa tahadhari

Spread the loveJUMLA ya watu watano wanaidaiwa kufariki dunia  katika vijiji vya...

Elimu

Harambee ujenzi sekondari za Musoma Vijijini yashika kasi

Spread the love  HARAMBEE ya ujenzi na ukarabati wa shule za sekondari...

Habari

Tanzania yaungana na nchi 180 kushiriki maonesho ya utalii Ujerumani

Spread the love  TANZANIA imeungana na mataifa 180 duniani kushiriki maonesho makubwa...

error: Content is protected !!