August 16, 2022

Uhuru hauna Mipaka

CBE chashika usukani shindano vyuo vikuu

Spread the love

CHUO cha Biashara (CBE) jijini Dar es Salaam kwa wiki hii ndicho kinachoongoza kwenye Shidano la Uwekezaji kwa Wanafunzi wa Vyuo Vikuu, anaandika Regina Mkonde.

Shindano hilo linadhaminiwa na Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) ambapo fainali zake zinatarajiwa kufanyika tarehe 2 Agosti mwaka huu.

Wakati akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Mary Kinabo, Ofisa Mwandamizi wa Masoko DSE amevitaja vyuo ambavyo wananfunzi wake wameingia katika nafasi ya 10 bora ikiwemo Chuo cha Maendeleo ya Mipango (IRDP), Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) na Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA).

“Shindano la Vyuo Vikuu (DSE Scholar Investment Challenge 2016),

Finali ya mwisho ya shindano itakuwa terehe 2 August 2016, vyuo vikuu ambavyo wanafunzi wake wameingi katika 10 bora ya fainali ya shindano ni vitano ikiwemo Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA),” amesema Kinabo.

Aidha, Kinabo amesema kuwa, idadi ya mauzo pamoja na mtaji wa soko kwa wiki iliyopita umeshuka na idadi ya hisa zilizonunuliwa imepanda mara tatu zaidi.  

“Idadi ya mauzo imeshuka kwa asilimia 49 na kufikia Tsh. 5.9 Bilioni kutoka Tsh. 11.6 Bilioni. Idadi ya hisa zilizouzwa na kununuliwa imepanda mara 3 zaidi hadi Sh. Milioni 5.4 kutoka Sh. Milioni 1.7,”amesema.

Amesema, kampuni tatu zinazoongoza kwa idadi ya hisa zilizouzwa na kununuliwa ni DSE kwa asilimia 61, CRDB asilimia 35, na TBL asilimia 2.6.

Ukubwa wa mtaji wa soko umeshuka kwa kiasi cha asilimia 2 na kufika Trilioni 23 kutoka Trillioni 23.3,Ukubwa wa mtaji wa makampuni ya ndani umepanda kwa asilimia 0.25 kufikia Trilioni 7.94 kutoka Trilioni 7.92,” amesema na kuongeza.

“Sekta ya viwanda (IA) wiki hii imepanda kwa pointi 11.47 baada ya bei za hisa za TCCL kupanda kwa asilimia 0.61 na TBL 0.44. Sekta ya huduma za kibenki na kifedha (BI) wiki hii imepanda kwa pointi 5.83 baada ya bei kupanda kwenye kaunta za DSE kwa asilimia 104 na NMB asilimia 1.18.

“Sekta ya huduma za kibiashara (CS) wiki hii imepanda pointi 29.30 baada ya bei kupanda kwenye kaunta ya SWISSPORT asilimia 1.11.”

error: Content is protected !!