December 1, 2021

Uhuru hauna Mipaka

CAS yatupilia mbali rufaa ya Yanga kwa Morrison

Spread the love

MAHAKAMA ya kimataifa ya usuluhishi wa michezo ‘CAS’ imetupilia mbali Rufaa ya klabu ya Yanga, dhidi ya mchezaji Bernad Morrison Raia wa Ghana na kumfanya mchezaji huyo kuwa halali kuitumikia klabu ya Simba. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)

Uamuzi wa mahakama hiyo, umetolewa leo tarehe 21, Novemba 2021, mwaka huu katika taarifa yao kwa vyombo vya habari mara baada ya kusikiliza shauri 29 Julai, mwaka huu kwa pande zote mbili kwa njia ya video kwa kuwasilisha vielelezo vya ushahidi.

Shauri hilo lilianza kusikilizwa mara baada ya CAS kuondoa pingamizi la awali (Preliminary Objection) lililowekwa na Bernard Morrison kwa kutaka kesi hiyo kusikilizwa nchini.

Kufuatia kuondolewa kwa pingamizi hilo Juni 2 mwaka huu, Mahakama hiyo ilitaka pande zote mbili kutuma mapendekezo ya namna gani kesi itasikilizwa, kwa kutumia njia ya nyaraka au maneno (mtandao).

Morrison aliingia kwenye mgogoro na klabu hiyo mara baada ya kujiunga na klabu ya Simba Agosti, 2020 huku klabu ya Yanga ikidai kuwa bado ilikuwa na mkataba na mchezaji huyo.

Kesi hiyo ilifika kwenye kamati ya Sheria na hadhi kwa wachezaji iliyokuwa chini ya Mwenyekiti wake Elias Mwanjala ambao walitoa maamuzi ya kuwa mchezaji huyo yupo huru na halali kuichezea klabu ya Simba.

Mara baada ya hapo klabu ya Yanga haikulizika na hukumu hiyo na kuamua kukimbilia kwenye mahakama hiyo ya kimataifa ya michezo.

Morrison alifika nchini kwa mara ya kwanza tarehe 15 Januari, 2020 na kujiunga na Yanga kwa mkataba wa miezi sita licha ya baadae klabu hiyo kudai kuwa mchezaji huyo aliongeza tena mkataba kwa miaka miwili.

Kwa sasa mchezaji huyo anakipiga kwenye klabu ya Simba toka msimu uliopita na kufanikiwa kutwaa taji la Ligi Kuu Tanzania Bara na kombe la Shirikisho la Azam.

error: Content is protected !!