MAHAKAMA ya usuluhishi wa michezo ya kimataifa (CAS) imetupilia mbali rufaa ya mchezaji Bernad Morrison dhidi ya Yanga kwenye kesi ya kimkataba kati ya pande hizo mbili. Anaripoti Kelvin Mwaipungu….(endelea)
Taarifa iliyotolewa na klabu ya Yanga iliyokuwa inazungumzia mwenendo wa kesi hiyo huku ikieleza sababu iliyopelekea kucheleweshwa usikilizwaji wa kesi hiyo ni kutokana na mchezaji huyo kuweka pingamizi la awali (Preliminary Objection) kwa kutaka kesi hiyo irudishwe nchini.
Mara baada ya pingamizi hilo kwa mujibu wa taarifa hiyo ya Yanga iliendelea kueleza kwamba CAS imetupilia mbali ombi hilo na kesi rasmi ya msingi itaanza kusikilizwa kuanzia tarehe 2 juni, 2021.
Mchezaji huyo aliingia kwenye mgogoro na klabu hiyo mara baada ya kujiunga na klabu ya Simba Agosti, 2020 huku klabu ya Yanga ikidai kuwa bado ilikuwa na mkataba na mchezaji huyo.
Kesi hiyo ilifika kwenye kamati ya Sheria na hadhi kwa wachezaji iliyokuwa chini ya Mwenyekiti wake Elias Mwanjala ambao walitoa maamuzi ya kuwa mchezaji huyo yupo huru na halali kuichezea klabu ya Simba.
Mara baada ya hapo klabu ya Yanga haikulizika na hukumu hiyo na kuamua kukimbilia kwenye mahakama hiyo ya kimataifa ya michezo.
Morriso alifika nchini kwa mara ya kwanza tarehe 15 Januari, 2020 na kujiunga na Yanga kwa mkataba wa miezi sita licha ya baadae klabu hiyo kudai kuwa mchezaji huyo aliongeza tena mkataba kwa miaka miwili.
Leave a comment