Wednesday , 8 February 2023
Home Kitengo Michezo Carabao Cup mguu mmoja mbele, Man U wamelala yooo!
Michezo

Carabao Cup mguu mmoja mbele, Man U wamelala yooo!

Spread the love

 

MICHUANO ya Carabao Cup inayoshirikisha timu za ligi kuu England na ligi za chini za nchini humo imezidi kupamba moto na kufikia hatua ya nne ambayo itajumuisha timu 16 zitakazochuana kutinga robo fainali. Anaripoti Damas Ndelema, TUDARCo … (endelea).

Timu hizo 16 zimepatikana baada ya kufuzu kutoka katika hatua ya tatu ya michuano hiyo inayochezwa kwa mechi moja tu isiyokuwa na marudiano.

Aidha, katika michuano hiyo, jana imeshuhudiwa mashetani wekundu – Manchester United waliokuwa nyumbani Old Traford wakifungashwa virago na klabu ya West Ham United kwa bao 1- 0.

Vigogo wengine kama Liverpool, Tottenham, Arsenal, Manchester city wamefuzu hatua hiyo lakini Chelsea wamefuzu kwa mbinde baada ya kuiondosha klabu ya Aston villa kwa mikwaju ya penalti baada ya sare ya bao moja kwa moja.

Aidha timu nyingine zilizofuzu katika hatua hiyo ni pamoja na Leicter city, Leeds, Southampton, West Ham, QPR, Stoke City, Brentford, Preston, Brighton, Sunderland na Burnley kukamilisha idadi ya timu hizo 16 zitakazoenda kuchuana katika raundi hiyo ya nne.

Pia katika raundi hiyo, timu hizo zitachuana ilikupata timu nane zitakazofuzu hatua inayofuata ya robo fainali ya michuano hiyo.

Tayari droo ya 16 bora imeshapangwa kama ifuatavyo; Chelsea Vs Southampton, Arsenal Vs Leeds, Westham Vs Manchester city, Stoke Vs Brentford, Leicester city Vs Brighton, Burnley Vs Tottenham, QPR Vs Sunderland, Preston Vs Liverpool.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

GGML: Uwanja mpya wa Geita Gold FC kukamilika Mei, 2023

Spread the loveUWANJA wa Magogo unaojengwa na Halmashauri ya Mji wa Geita...

Michezo

Wanafunzi chuo Mwalimu Nyerere wapongezwa kwa ushindi

Spread the love  UONGOZI wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (MNMA)...

Michezo

Arsenal waipopoa Manchester United

Spread the loveKLABU ya Arsenal inayoshiriki Ligi Kuu England imewatandika Mashetani Wekundu...

Michezo

Mchezaji Singida apoteza maisha mazoezini

Spread the love  MCHEZAJI na kapteni wa timu ya vijana ya Singida...

error: Content is protected !!