Tuesday , 27 February 2024
Home Kitengo Michezo Cameroon walivyo thibitisha ubora wao AFCON
Michezo

Cameroon walivyo thibitisha ubora wao AFCON

Timu ya Taifa ya Cameroon wakishangilia baada ya kutwaa ubingwa wa AFCON 2017
Spread the love

BAADA ya kukamilika kwa michuano ya kombe la mataifa Afrika iliokuwa inafanyika nchini Gabon, na timu ya taifa ya Cameroon kufanikiwa kutwaa ubingwa huo kwa mara ya tano katika historia ya michuano hiyo, baada ya kuifunga Misri kwa mabao 2-1.

Licha ya kutwaa ubingwa huo lakini mabingwa hao waliweza kuoneasha ubora wao katika mchezo wa fainali baada ya kumtoa Benjamin Moukandjo kuwa mchezaji bora wa mechezo wa fainali.

Haikuishia hapo tu, Cameroon walifanikiwa kumtoa Christian Bassogog kuwa mchezaji bora wa michuano hiyo iliyo malizika jana, baada ya kuonekana kuwa mchezaji alioibeba timu yake kwa asilimia kubwa katika fainali hizo.

Ubora mwengine waliouonesha mabingwa hao katika michuano hiyo, ni jinsi walivyopambana na timu vigogo mpaka kufikia hatua ya kutwaa ubingwa, baada ya kuitoa Senegal katika hatua ya robo fainali kwa njia ya mikwaju ya Penati.

Katika hatua ya nusu fainali, Cameroon walichuana na Ghana kwa mabao 2-0 licha ya Ghana kupewa nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa, kutokana na kuwa na kikosi kipana kilicho sheheni wachezaji wengi wenye uzoefu na michuano hiyo kwa muda mrefu.

Mchezo wa jana wa fainali ulikuwa ni kama Cameroon walikuwa wanalipa kisasi dhidi ya Misri, baada ya kupoteza katika mchezo wa fainali uliofanyika mwaka 2008 nchini Ghana, baada ya kufungwa bao 1-0 na mfungaji akiwa Mohamed Aboutrika.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Wizara yaahidi kuboresha, kuimarisha michezo

Spread the loveIkiwa ni saa kadhaa baada ya kumalizika kwa mashindano ya...

Habari MchanganyikoMichezo

Nje jogging yanyakua medali 20 Kili Marathon

Spread the loveTimu ya riadha ya Wizara ya Mambo ya Nje na...

Michezo

Siku ya kukusanya maokoto ni leo, usipange kukosa

Spread the love  HATIMAYE Jumamosi imefika ndugu mteja wa Meridianbet na mechi...

Michezo

Kuwa milionea na Meridianbet ni rahisi sana

Spread the love  JE, unajua kuwa leo hii ni siku nzuri kwako...

error: Content is protected !!