January 17, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Cameroon, Cape Verde waanza vema michuano AFCON

Spread the love

 

WENYEJI wa mashindano ya Kombel la Mataifa ya Afrika, Cameroon jana usiku walitoka nyuma na kuwalaza Burkina Faso bao 2-1 katika mechi ya ufunguzi iliyokuwa imesheheni matukio mbalimbali kuhusu mashidano hayo. Anaripoti Mwandishi Wetu .. (endelea)

Cameroon waliokuwa wakishajihishwa na mashabiki wao pamoja na Rais wa nchi hiyo, waliduwazwa na bao la mapema dakika ya 24 baada ya Gustavo Sangare kuifanya Burkina Faso kutangulia kwa bao la mapema katika kipindi cha kwanza huko Yaounde.

Hata hivyo, penalti mbili kutoka kwa nahodha Vincent Aboubakar ziligeuza mchezo huo kuwa faida kwa wenyeji kabla ya muda wa mapumziko.

Kipa wa ‘Indomitable Lion’s (Cameroon), Andre Onana aliokoa mabao mawili ya wazi kipindi cha pili na kuwafanya vijana hao wa Kocha Toni Conceicao kufungua pazia la Kundi A kwa ushindi.

Katika mchezo uliofuata, Timu ya Taifa ya Cape Verde iliyokumbwa na visa vya Covid-19 iliilaza Ethiopia bao 1-0.

Katika mchezo huo wa pili uliopigwa kwenye Uwanja wa Olembe, Ethiopia walibaki 10 uwanjani baada ya mchezaji wao kupata kadi nyekundu.

Cape Verde walihaha vilivyo na hadi mshambuliaji Julio Tavares alipofunga bao la kichwa dakika za lala salama.

Michezo minne leo inatarajiwa kupigwa ambapo saa 10:00 jioni Senegal watavaana na Zimbabwe, saa moja usiku Morocco watakipiga na Ghana, Guinea watapepeta na Malawi wakati saa nne usiku Comoro watamenyana na Gabon.

error: Content is protected !!