Friday , 2 June 2023
Home Gazeti Habari za Siasa CAG vs Spika Ndugai: LHRC yamwandikia barua Waziri Mkuu
Habari za Siasa

CAG vs Spika Ndugai: LHRC yamwandikia barua Waziri Mkuu

Prof. Mussa Juma Assad, Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG)
Spread the love

KITUO cha Sheria na Haki za Binadamu Tanzania (LHRC) kimetoa wito kwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kuingilia kati mvutano uliopo kati ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad na Bunge. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

LHRC tarehe 18 Aprili 2019 imemuandikia barua ya wazi Waziri Majaliwa, ikimtaka aishauri serikali kupitia Baraza la Mawaziri na Bunge kupitia vikao vyake rasmi, kutengua uamuzi wa mhimili huo wa kutofanya kazi na Prof. Assad.

Sehemu ya barua hiyo ya wazi ya LHRC kwa Waziri Majaliwa, inaeleza kwamba, kitendo cha bunge kufikia uamuzi wa kujitenga na Prof. Assad kinaleta mgogoro wa kikatiba na uwajibikaji wa maslahi ya Taifa.

Pia, inaeleza kwamba mgogoro huo umeleta sintofahamu kwa watetezi wa haki za binadamu katika suala la uwajibikaji na utawala bora, na kwamba kwa kuwa Waziri Majaliwa ni Mtendaji Mkuu wa Serikali na Kiongozi wa shughuli za serikali bungeni ni vyema akaingilia kati suala hiyo.

“Katika hili, tunaamini kwamba kwa kuwa Waziri Mkuu ndiyo Mtendaji Mkuu wa Serikali na Kiongozi wa shughuli za Serikali Bungeni ni vema kuishauri Serikali kupitia Baraza la Mawaziri na Bunge kupitia vikao rasmi vya Bunge, kutengua maamuzi yake ya kutofanya kazi na CAG ili kuondoa mgogoro wa Kikatiba unaotengenezwa.

“Pamoja na kulinda dhana ya uwajibikaji wa maslahi ya Taifa. Mvutano huu pia unalenga kudhoofisha juhudi za mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli za kupambana na ubadhirifu serikalini,” inaeleza sehemu ya barua ya LHRC.

Aidha, LHRC imemtaka Waziri Majaliwa kuhimiza wakuu wa wizara na taasisi za serikali zilizotajwa ndani ya Ripoti ya Prof. Assad kutekeleza mapendekezo ya mdhibiti huyo ili kuongeza uwajibikaji wa fedha za umma.

Kituo hicho kimeeleza kuwa, utekelezaji wa mapendekezo CAG katika kipindi cha miaka miwili umeshuka kwa asilimia 4, na kwamba hali hiyo ni tishio dhidi ya uwajibikaji wa taasisi za serikali hususan katika kuhakikisha mipango na matumizi halali ya fedha za umma kama ilivyopitishwa katika bajeti kuu za serikali.

“Ofisi yako ifanye jitihada za makusudi kusukuma uwajibikaji wa matumizi ya fedha kulingana na mapendekezo ya ripoti hiyo, pia itoe wito na agizo la kuwachukulia hatua za kinidhamu, kiutawala ama za kijinai watu wote waliyohusika katika matumizi ya fedha yaliyo kinyume na viwango vya ukaguzi kwa mujibu wa sheria za nchi na mapendekezo ya CAG,” inaeleza sehemu ya barua hiyo ya LHRC.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Lusinde: CCM hatuliachii ng’o jimbo la Moshi Mjini

Spread the loveMJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (NEC), Livingston...

Habari za SiasaTangulizi

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar: Bakharesa hajavamia shamba letu

Spread the love  IKULU Visiwani Zanzibar, imeeleza kuwa eneo la kiwanda cha...

Habari za SiasaTangulizi

Zanzibar watangaza rasmi kuwa shamba la Razaba ni mali yao

Spread the love  SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), imetangaza rasmi kwamba shamba...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Mwinyi azindua Kamati ya Maridhiano Visiwani

Spread the love  RAIS wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Dk. Hussein...

error: Content is protected !!