RIPOTI za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), kwa mwaka 2019/20, zimewasilishwa bungeni jijini Dodoma huku taasisi kumi zikipata hata mbaya na 81 zenye shaka. Anaripoti Regina Mkonde…(endelea).
Ripoti hizo, zimewasilishwa leo Alhamisi tarehe 8 Aprili 2021, na CAG Charles Kichere.
Kichere amewasilishwa jumla ya ripoti 21 zinazojumuisha masuala mbalimbali yaliyojitokeza katika ukaguzi alioufanya kwa Mwaka wa Fedha ulioishia tarehe 30 Juni 2020 kwa taasisi nilizozikagua.
CAG huyu amesema, “kwa mwaka huu, nimetoa hati mbaya kwa kumi” huku taasisi 82 zikipata hati zenye shaka.
Amezitaja taasisi hizo kumi kuwa ni; Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga, Halmashauri ya Wilaya ya Singida, Halmashauri ya Wilaya ya Itigi, Halmashauri ya Wilaya ya Igunga na Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge.
Zingine ni; Halmashauri ya Wilaya ya Urambo, Halmashauri ya Wilaya ya Momba, Halmashauri ya Manispaa ya Tabora, Tume ya UNESCO na Hospitali ya Rufaa ya Mkoa, Morogoro.
Taasisi 81 zilizopata hati zenye shaka hizi hapa chini, zikiwemo vyama vya siasa, vyuo vikuu, halmashauri na wakala.
Leave a comment