Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa CAG awasili bungeni, mfumo wa kumhoji ni huu
Habari za SiasaTangulizi

CAG awasili bungeni, mfumo wa kumhoji ni huu

Prof. Mussa Assad, Mkaguzi na Mdhabiti wa Hesabu za Serikali (CAG) akiwasili katika viwanja vya Bunge, jijini Dodoma
Spread the love

PROFESA Mussa Assad, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) amewasili bungeni kuitikia wito uliotolewa na Job Ndugai, Spika wa Bunge la Jamhuri wa kukutana na Kamati ya Maadili ya Bunge. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Prof. Assad amewasili katika viwanja vya Bunge majira ya saa 4:45 asubuhi ya leo Jumatatu ya tarehe 21 Januari, 2019, tayari kwa mahojiano mbele ya mwenyekiti wa kamati hiyo na kisha kuanza kuhojiwa na wajumbe.

Swali lolote atakaloulizwa kutoka kwa mjumbe yoyote, atatakiwa kulijibu kwa kumuelekea mwenyekiti na sio muuliza swali.

Baada ya mahojiano hayo, Prof. Assad atatakiwa kutoka nje ya ukumbi wa mahojiano ili kutoa nafasi kwa mwenyekiti na wajumbe wa kikao hicho ili kupitia maelezo yake na kama kuna maelezo ya ziata wanayoweza kuyataka kutoka kwake.

Baada ya kikao kupitia nukta kwa nukta na kujiridhisha, Prof. Assad ataitwa tena kwenda kwenye kikao hicho ili kumalizia hatua ya mwisho.

Baada ya kumaliza kikao hicho, itapeleka ripoti yake kwa Spika ikiwa pamoja na mapendekezo yake dhidi ya mtuhumiwa. Spika naye atakuwa na hiyari ya kusoma bungeni uamuzi uliofikiwa ama wabunge kupendekeza adhabu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

error: Content is protected !!