Friday , 19 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa CAG amng’ang’ania Spika Ndugai
Habari za SiasaTangulizi

CAG amng’ang’ania Spika Ndugai

Prof. Mussa Juma Assad, Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG)
Spread the love

PROF. Mussa Assad, Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), apigilia msumali kauli yake kuwa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, halina meno na “ni dhaifu.” Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dar es Salaam, leo (Alhamisi), tarehe 17 Januari 2019, Prof. Assad amesema, bado anaendelea kusimamia msimamo wake kuwa Bunge la Tanzania linaloongozwa na Job Ndugai, ni dhaifu na kwamba maneno hayo, ni ya kawaida kwa wakaguzi wa mahesabu.

Anasema, “hii ni lugha ya kawaida sana kwa wakaguzi wanapotoa maoni yangu. Hivyo hakuna kokote ambako nimedhalilisha Bunge. Bado nitaendelea kusimamia maneno hayo.”

Anasema, “majibu yangu katika mahojiano niliyofanya nikiwa nchini Marekani na ambayo yamezua mjadala huu, hayakuwa na nia ya kulidhalilisha Bunge hata kidogo. Maneno kama udhaifu, ni lugha ya kawaida sana kwa wakaguzi kutoa maoni ya utendaji wa mfumo wa taasisi mbalimbali.”

Kauli ya Prof. Assad imekuja kufuatia Spika Ndugai kutoa amri ya kumtaka kufioka mbele ya Kamati ya Haki, Kinga, Maadili na Madaraka ya Bunge, ili kuhojiwa juu ya kauli yake hiyo.

Spika huyo wa Bunge alinukuliwa na vyombo vya habari akiwa mjini Dodoma akimtuhumu kiongozi huyo, kudhalilisha mhimili huo wa Bunge.

Prof. Assad anatakiwa kufika kwa hiari yake mbele ya kamati hiyo, tarehe 21 Januari 2019.

Wiki iliyopita, CAG alilimbia MwanaHALISI Online kuwa alitegemea Spika Ndugai kuwa mtu wa kwanza wa kuheshimu Katiba ya Nchi. Alisema, alichokieleza katika mahojiano yake hayo ambayo “yamezua mtafaruku” kati ya ofisi yake na Spika Ndugai, hayakupaswa kupewa uzito unaopewa.

Anasema, “…Ibara ya 18 (a) inampa kila mtu uhuru wa kutoa maoni. Hivyo basi, kwangu mimi nayachukulia hayo yote, kama mtu kaamua kutoa maoni yake na kuelezea fikra zake.

“Ibara ya 26 (1), ya Katiba ya Jamhuri, inaelezea wajibu wa kila mtu kufuata na kutii katiba ya nchi. Spika anapaswa kuwa mfano bora katika kuhakikisha kuwa Ibara ya 143 ya Katiba, inayonitambua mimi na taasisi ninayoingoza, inaheshimiwa kama inavyostahiki.”

Katika mkutano wake na waandishi wa habari leo, CAG anaendelea kusisitiza msimamo wake. Hata hivyo, anasema atafika mbele ya Kamati ya Bunge kuitikia wito huo.

Anasema amepokea wito rasmi wa maandishi, tarehe 15 Januari 2019 unaomtaka kufika mbele ya Kamati ya Kudumu ya Maadili. Anasema, “kwa mantiki ya kudumisha mahusiano mazuri kati ya ofisi yangu na Bunge… ninayo nia ya kuitikia wito huo.”

Prof. Assad ameeleza kusikitishwa kwake kwa namna kauli yake ya kiukaguzi ilivyotafsiriwa na hatimaye kuzua mjadala.

Anasema,“mimi na Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi hatuna namna ya kuathiri tafsiri za viongozi, wanasiasa na wachangiaji wa kawaida, tunachoshauri ni uungwana utawale katika mawasiliano yetu.

Anaongeza, “yametokea malumbano makali sana kuhusiana na ile kauli, lakini sisi Ofisi ya Mkaguzi tunashauri uungwana utawale na hatufurahishwi na yanayoendelea sasa,” amesema Prof. Assad.

Amesema, ofisi yake na Bunge ni lazima zifanye kazi kwa ukaribu na kwa maelezo mazuri ili kuwepo ushirikiano mzuri.

Akizungumzia mahojiano yake na Mwandishi Anord Kayanda wa Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa yaliyofanywa hivi karibuni n ahata kuzua mjadala, hakuwa na nia ya kudhalilisha Bunge.

“Majibu yangu katika mahojiano yaliyozua mjadala hayakuwa na nia ya kulidhalilisha Bunge hata kidogo, maneno kama udhaifu ni lugha ya kawaida sana kwa wakaguzi kutoa maoni ya utendaji wa mfumo wa taasisi mbalimbali,” amesisitiza Prof. Assad.

Wachambuzi wa masuala ya kikatiba wanasema, hatua ya Spika Ndugai kumuita CAG na hatua ya kiongozi huyo kuitikia wito huo, ni kuzidi kuvunja Katiba.

Tangu Spika Ndugai kutoa wito huo, watu kadhaa akiwamo Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Fatma Karume, wamepinga hatua hiyo wakisema, inakwenda kinyume na Katiba.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari za Siasa

Mavunde aagiza Perseus kuharakisha fidia Sengerema

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameipongeza Kampuni ya Perseus kwa...

Habari za Siasa

Kigogo Chadema awanyooshea vidole vigogo serikalini kuhusu ripoti ya CAG

Spread the love  MJUMBE wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na...

Habari za Siasa

Wabunge waikalia kooni TAKUKURU Bungeni

Spread the love  BAADHI ya wabunge wamelia na changamoto za utendaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Mpina ataka Waziri Majaliwa ajiuzulu, akosoa teuzi za mawaziri

Spread the love  MBUNGE wa Kisesa, Luhaga Mpina, amemtaka Waziri Mkuu, Kassim...

error: Content is protected !!