FEDHA zilizotolewa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) na kutumika kati ya Januari na Machi mwaka huu, zimeanza kuchunguzwa. Anaripoi Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Hatua hiyo inatokana na agizo la Rais Samia Suluhu Hassan, kuagiza Ofisi ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takururu) pia Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), kupitia mafaili ya matumizi ya fedha hizo.
Rais Samia alitoa maagizo hayo tarehe 28 Machi 2021, wakati akipokea taarifa ya CAG na ya utendaji wa Takukuru kwa mwaka 2019/2020.

Akizungumza na gazeti moja la kila siki nchini, CAG Charles Kichere amesema, tayari wameanza uchunguzi BoT ikiwa ni kutekeleza agizo la Rais Samia.
“Tunaendelea na ukaguzi. Siwezi kusema kilichofanyika hadi sasa tupo site (eneo la tukio), tunaendelea na ukaguzi,” CAG Kichere amelieleza gazeti hilo.
Leave a comment