August 16, 2022

Uhuru hauna Mipaka

CAG akamata taasisi 13

Spread the love
RIPOTI ya Prof. Mussa Juma Assad, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), imebaini taasisi 13 za serikali zilizofanya matumizi nje ya bajeti iliyopangwa,anaripoti Aisha Amran.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, taasisi hizo zimefanya matumizi nje ya bajeti na kugharimu Sh. 1,298,373,921 katika ukaguzi wa hesabu  za  mwaka 2014/15.
Taasisi hizo ni balozi tisa,  wizara  mbili  na sekretarieti  mbili za  mikoa  ambazo zimelipa kiasi  hicho cha fedha kwa matumizi  mbalimbali nje  ya  bajeti  iliyoidhinishwa bila kutafuta idhini au kibali kinyume na Kanuni 46 (3) ya Kanuni za Fedha za Umma ya Mwaka 2001 (Iliyorejewa 2004).
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, baadhi  ya  shughuli zilizopangwa  hazikuweza  kutekelezwa  kama ilivyoidhinishwa  kwenye  bajeti.
Ripoti hiyo ya imebainisha kwamba Jumla  ya  matumizi hayo,  kiasi  cha  Shilingi 147,662,326 kilikuwa matumizi nje ya  bajeti na  Shilingi 1,150,711,595 kilikuwa  ni matumizi zaidi ya kiasi kilichoidhinishwa.
Taasisi hizo 13 zilizofanya malipo nje ya matumizi ya bajeti na kiasi chake kwenye mabano ni ubalozi wa Tanzania Pretoria, Afrika Kusini ilikuwa (Sh. 27,813,874),Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi (Sh. 5,000,000).
Ubalozi wa Tanzania Addis Ababa, Ethiopia (Sh. 103,494,252), Sekretarieti ya Mkoa wa Shinyanga (11,354,200), Ubalozi wa Tanzania, Pretoria, Afrika ya Kusini (Sh. 200,726,900), Ubalozi wa Tanzania-Maputo, Msumbiji (Sh. 146,847,102), Ubalozi wa Tanzania-Moroni, Comoro (Shilingi 374,890,135).
Nyingine ni Ofisi ya Waziri Mkuu (Shilingi 15,165,515), Ubalozi wa Tanzania- Lilongwe (Sh. 42,902,594), Ubalozi wa Tanzania-Beijing, China (Sh. 109,448,872), Ubalozi wa Tanzania-Moscow, Urusi (Shilingi 97,557,289), Ubalozi wa Tanzania-Rome, Italia (Sh.154,733,188), Sekretarieti ya Mkoa –Lindi.
error: Content is protected !!