Thursday , 28 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa CAG ahofia CCM kupoteza bilioni 3, kesi 108 kortini
Habari za SiasaTangulizi

CAG ahofia CCM kupoteza bilioni 3, kesi 108 kortini

Daniel Chongolo, Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM)
Spread the love

 

MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) nchini Tanzania, Charles Kichere ameonesha hofu kwa wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya kupata hasara ya Sh.3.63 bilioni kama itashindwa katika kesi 108 zilizopo mahakamani. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Katika ripoti ya CAG Kichere ya Serikali Kuu kwa mwaka 2022/21 aliyowasilishwa bungeni jijini Dodoma Jumanne hii amesema, amepitia majalada ya kisheria ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na kugundua CCM kina kesi 108 zilizofunguliwa na wadai mbalimbali kwenye mahakama tofauti.

Amesema, kati ya kesi zilizofunguliwa, kesi 86 zinahusu migogoro ya ardhi, kesi 12 zinahusu kazi na kesi 10 zinahusu madai zenye thamani ya Sh. bilioni 3.63.

CAG Kichere amesema, kikubwa zaidi, nilibaini CCM kina kiwango kikubwa cha kesi za ardhi ikilinganishwa na kesi zingine zilizo katika ngazi tofauti za mahakama, zenye mamlaka ya kuamua migogoro ya ardhi kama ilivyobainishwa katika Kifungu cha 3(1) na (2) cha Sheria ya Mahakama ya Migogoro ya Ardhi Sura ya 216.

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) nchini Tanzania, Charles Kichere

Amesema katika ukaguzi, wangu nilibaini kuwa kasi ya ongezeko la kesi za ardhi inachangiwa na kuchelewa katika kutatua migogoro ya ardhi kutokana na kukosekana kwa mfumo mzuri wa utatuzi wa migogoro ya ardhi ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM).

CAG huyo amesema, menejimenti ya CCM ilifafanua kuwa walikuwa na kesi na mashauri 112 zenye jumla ya Sh. bilioni 4.14 mwaka jana ikilinganishwa na kesi 108 zenye thamani ya Sh. Bilioni 3.63 mwaka huu.

Amesema kwa hali hiyo, kumekuwa na uboreshaji ikilinganishwa na mwaka uliopita.

“Pamoja na kwamba CCM kinaonesha kuwa na kesi ndogo mwaka huu ikilinganishwa na mwaka jana, lakini ni maoni yangu kuwa kesi zilizofunguliwa dhidi ya CCM, zikitolewa hukumu zitazofaidisha upande wa walalamikaji, kunaweza kuwa na hasara ya Sh. bilioni 3.63 kwa wanachama wa CCM na washirika wake,” amesema CAG Kichere na kuongeza:

“Ninapendekeza CCM ianzishe mfumo wa utatuzi wa migogoro na kuboresha vya kutosha kitengo chake.”

2 Comments

  • Duh!
    CCM inanikatisha tamaa. Tunagombania ardhi na wananchi. Kwa nini tunahitaji ardhi wakati tunasimamia SERA.
    Jamani, tunatumia siasa kujimilikisha ardhi.
    Naomba zirejeshwe na ofisi ziishie wilayani. Kwa maana hiyo, tuwe na ofisi ya taifa, mkoa, na wilaya tu.

  • During magufuli’s tenure, ccm leaders embarked on land and property grabbing. Bus stations, sports stadiums, small farms in villages to name a few. It was only possible because of who was in power. Now he is gone, Bashiru is not there either and tanzanians feel may be they can get haki in the courts.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Alichokisema Rais Samia baada ya kupokea ripoti ya CAG, TAKUKURU

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Serikali yake itafanyia kazi...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga kuongoza usambazaji wa mitungi ya gesi 10,000 ya Taifa Gas

Spread the loveNaibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga ameahidi kuongoza kwa ufanisi...

Habari za SiasaTangulizi

Deni la Serikali laongezeka kwa trilioni 11

Spread the loveDENI la Serikali imeongezeka kwa takribani Sh. 11 trilioni sawa...

Habari za SiasaKimataifa

Mwanaye rais jela miaka miaka 6 kwa dawa za kulevya

Spread the loveMwanawe rais wa zamani wa Guinea-Bissau amehukumiwa kifungo cha miaka...

error: Content is protected !!