May 20, 2022

Uhuru hauna Mipaka

CAG abaini ubadhirifu bilioni 23.8 h/mashauri 59, atoa maagizo Takukuru

Ofisi za Jiji la Dar es Salaam

Spread the love

 

MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Charles Kichere, amebaini ubadhirifu wa Sh.23.8 bilioni, katika halmashauri 59. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

CAG Kichere amebainisha ubadhirifu huo leo Alhamisi tarehe 8 Aprili 2021, wakati anatoa muhtasari wa ripoti yake ya ukaguzi kwa mwaka 2019/2020, jijini Dodoma.

Akielezea ubadhirifu huo, amesema umefanyika kuanzia mwaka 2017/18 hadi 2019/2020, ambapo kiasi hicho cha fedha, zilikuwa makusanyo ya mawakala kupitia mfumo wa kielektroniki wa ukusanyaji mapato ya Serikali (LGRCIS), hazikuwasilishwa benki.

“Matokeo ya ukaguzi uliofanyika katika mamlaka 59 za serikali za mitaa, yanaonesha kwa kipindi hicho, makusanyo ya jumla ya Sh.23.8 bilioni kutoka vyanzo mbalimbali vya mapato ya ndani yalibainika kutowasilishwa benki kutokana na udhaifu wa mfumo wa udhibiti wa ndani,” amesema CAG Kichere.

Charles Kichere, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG)

Kufuatia ubadhirifu huo, CAG Kichere ameshauri mamlaka husika kushirikiana na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), kuwachukulia hatua watu waliohusika na ubadhirifu huo.

Miongoni mwa Halmashauri zilizoguswa na ubadhirifu huo ni, Halmashauri ya ilaya Kinondoni iliyopoteza Sh.5.98 bilioni, Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kabla halijavunjwa (Sh.1.6 bilioni), Halmashauri ya Jiji la Arusha (Sh.1.2 bilioni) na Halmashauri Wilaya ya Songea (Sh.1 bilioni).

Nyingine ni, Halmashauri ya Wilaya ya Chemba (Sh.769.1 milioni) Halmashauri Wilaya ya Itilima (Sh.714.4 milioni), Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa (Sh.713.6 milioni) na Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu (Sh.612.8 milioni).

“Kwa maoni yangu, haya ni mapato halisi ya Serikali yaliyochepushwa na kutumiwa kwa matumizi binafsi kwa njia ya ubadhilifu. Nashauri mamlaka husika washirikiane na Takukuru. Kuhakikisha wahusika wanawajibika kurejesha fedha walizochukua au wanafikishwa kwenye vyombo vya sheria kujibu mashitaka,” ameshauri CAG Kichere.

Halmashauri zote hizi hapa chini;

error: Content is protected !!