November 29, 2021

Uhuru hauna Mipaka

CAF waiondoa Biashara United kombe la Shirikisho

Spread the love

 

MARA baada ya kushindwa kwenda kucheza mchezo wa marudiano nchini Libya dhidi ya Al Ahly Tripol, kamati ya mashindano ya Shirikisho la Mpira Barani Afrika “CAF” imeiondoa timu ya Biashara united kwenye michuno ya kombe la Shirikisho, kufuatia sababu walizotoa kutokuwa na mashiko. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)

Mechi hiyo ya marudiano ilipangwa kuchezwa tarehe 23, Oktoba 2021, nchini Libya mara baada ya mchezo wa awali ulipigwa Dar es Salaam, Biashara United ilifanikiwa kupata ushindi wa mabao 2-0.

Taarifa ya kuondolewa kwenye michuano hiyo kwa Biashara United, imetolewa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania ‘TFF’ ambapo hapo awali ndio waliochukua dhamana ya kuandika baraua kwenda Caf, mara baada ya timu hiyo kukwama.

Katika taarifa hiyo ya Tff ilieleza kuwa, CAF kupitia kamati yake ya mashindano, iliona sababu zilizoelezwa kupelekea mchezo huo kutofanyika hazikutokana na dharura.

Timu hiyo ilishindwa kutokea kwenye mchezo huo, mara baada ya kushindwa kusafiri huku sababu kubwa ikielezwa ni kukosa vibari vya ndege kutua nchini humo, mara baada ya kuikodi.

Timu hiyo ilikuwa ilipata kushiriki michuano hiyo kwa mara ya kwanza, kufuatia Tanzania kupata ushiriki wa timu nne kwenye michuano ya kimataifa kwa msimu huu wa 2021/22.

 

error: Content is protected !!