HALIDI Mchanga, Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Naliendele, amesimamishwa kazi kwa kushindwa kukamilisha mradi wa bweni na bwalo la chakula katika shule hiyo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Mtwara … (endelea).
Hatua hiyo imechukuliwa na David Silinde, Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), baada ya kutembelea shule hiyo iliyopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara Mikindani, Mtwara.
Silinde amesema, kwenye shule hiyo amekuta matumizi mabaya ya fedha ambazo zilipaswa kuelekezwa kwenye ujenzi huo uwe ambao ulipaswa kukamilika mwishoni mwa mwaka jana 2020.
Waziri huyo amesema, ujenzi huo umesimama licha ya Sh. 180 milioni zilizotolewa na serikali kuelezwa kwamba zimekwisha.
Mchanga amemweleza Silinde kwamba walikutana na changamoto ya upatikanaji wa saruji, mvua kubwa kukwamisha ujenzi.
Na kwamba, walilazimika wasubiri mvua ziishe mwanzoni mwa mwaka huu, pia ameeleza ushiriki hafifu wa wananchi katika kuchangia ujenzi ikiwemo kuchimba msingi, kumechangia.
Leave a comment