Saturday , 13 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Bwege, Vigogo wa CUF wahamishiwa Lindi
Habari za SiasaTangulizi

Bwege, Vigogo wa CUF wahamishiwa Lindi

Suleiman Bungara 'Bwege'
Spread the love

JESHI la Polisi limewasafirisha viongozi watatu waandamizi wa Chama cha Wananchi (CUF), waliowakamata juzi jioni baada ya kampeni za udiwani kwenye kata Kivinje kutoka kilwa mpaka Lindi. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Viongozi hao wamekamatwa kwa tuhuma ya kufanya uchochezi kwenye mkutano huo wa kampeni za uchaguzi wa marudii kwenye hiyo.

Miongoni mwa waliokamatwa, ni pamoja na Suleman Bungara ‘Bwege,’mbunge wa chama hicho katika jimbo la Kilwa Kusini.

Wengine, ni Naibu Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano wa chama hicho, Mbarala Maharagande, mwenyekiti wa Halmashauri ya Kilwa, Abuu Mjaka na mjumbe wa Kamati Tendaji, Fatuma Karambwe.

Bwege, mmoja wa wanasiasa wenye ushawishi mkubwa katika eneo hilo, alikamatwa na wenzake hao, muda mfupi baada ya kumaliza kuhutubia mkutano wa uzinduzi wa kampeni za udiwani kwenye kata ya Kivinje, wilayani Kilwa.

Taarifa zilizothibitishwa na Kaimu naibu katibu mkuu wa chama hicho, Tanzania Bara, Joran Bashange, viongozi licha ya kufikishwa kituo cha polisi, wameshindwa kupewa dhamana.

“Ni kweli kwamba mbunge wetu wa Kilwa Kusini, Sulemani Bwege na viongozi wengine wawili, Maharagande na Mjaka, wamekamatwa na mpaka sasa, bado wanaendelea kushilikiwa na jeshi la polisi,” ameeleza Bashange.

Anasema, “tukio hilo limetokea jana jioni, mara baada ya kumfunga mkutano wa ufunguzi wa kampeni za udiwani kwenye kata ya Kivinje.”

Jana akiongea kwa uchungu na MwanaHALISI Online, Bashange anasema, “huu ni uonevu mkubwa. Haukubariki kwa vigezo vyovyote vile vya kisheria na kiutu.”

Anasema, aliyeanza kushikiliwa na polisi, ni Maharagande na kwamba Bwege na Mjaka walipopata taarifa hizo, waliamua kwenda kufuatilia, ndipo nao wakakamatwa na kuwekwa ndani.

Uchaguzi mdogo wa udiwani katika kata ya Kivinje, unafanyika kufuatia aliyekuwa diwani wa kata hiyo, Jafari Arobaini, kuamua kujiuzulu.

Arobaini alitangaza kujiuzulu, mwezi mmoja uliyopita, kwa kile alichokiita, “kumuunga mkono Rais John Magufuli katika juhudi zake za kuiletea Tanzania maendeleo.”

Bwege amekuwa mmoja wa wabunge wanaojenga hoja za nguvu zinazoikosoa serikali ya Rais Magufuli bungeni na kuituhumu kwa mambo kadhaa, ikiwamo “mauwaji, utekaji na utesaji.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Dk. Nchimbi aanika ugonjwa wa CCM

Spread the loveKATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Emanuel Nchimbi,...

Habari za Siasa

Chadema yapuliza kipyenga uchaguzi viongozi kanda

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeanza maandalizi ya uchaguzi...

Habari za Siasa

CCM :Hatutaki ushindi wa makandokando uchaguzi Serikali za mitaa

Spread the loveCHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimesema hakihitaji ushindi wa makandokando katika...

Habari za Siasa

Makala: Puuzeni wanasiasa wanaojigamba wanaweza kubadili maamuzi ya mahakama

Spread the loveKATIBU wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),...

error: Content is protected !!