Friday , 19 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Bwege aalikwa kumpigia kampeni Raila Odinga
Habari MchanganyikoTangulizi

Bwege aalikwa kumpigia kampeni Raila Odinga

Spread the love

MBUNGE wa zamani wa Jimbo la Kilwa Kusini Selemani Said Bungara (Bwege) amealikwa nchini Kenya kumpigia kampeni mgombea wa Azimio la Umoja, Raila Odinga. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Taarifa hiyo imetolewa leo Alhamisi tarehe 4 Agosti, 2022 na Janeth Rithe, Katibu wa Habari, Uenezi na Mahusiano na Umma, ACT Wazalendo.

Bwege ambaye mwaka 2020 aligombea ubunge kupitia Chama cha ACT-Wazalendo na kuangushwa na mpinzani wake wa Chama cha Mapinduzi, amewasili nchini humo kwa ndege Air Tanzania mapema leo.

“Bwege ndio Mwanasiasa wa kwanza kutoka Tanzania kupewa heshima hiyo na Timu ya Kampeni ya Azimio la Umoja,” ikiwa ni wiki ya lala salama kabla ya uchaguzi mkuu kufanyika wiki ijayo tarehe 9 Agosti, 2022.

“Kumbukumbu za mtandaoni zinaonesha kuwa hotuba za Bwege ndani na nje ya Bunge zinafuatiliwa na kupendwa sana nchini Kenya,” amesema Rithe.

Mvuto wa Bwege kwa Wakenya wengi inaweza kutumika  kama karata ya mwisho kwenda kuongeza kura za Odinga.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Mpina ataka Waziri Majaliwa ajiuzulu, akosoa teuzi za mawaziri

Spread the love  MBUNGE wa Kisesa, Luhaga Mpina, amemtaka Waziri Mkuu, Kassim...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Habari za SiasaTangulizi

Tanzania, Uturuki zanuia kukuza biashara, uwekezaji

Spread the loveSERIKALI za Tanzania na Uturuki zimekubaliana kuendeleza dhamira ya kuimarisha...

error: Content is protected !!