Wednesday , 29 March 2023
Home Gazeti Habari Mchanganyiko Bwala la Nyerere kujaa kwa misimu miwili
Habari Mchanganyiko

Bwala la Nyerere kujaa kwa misimu miwili

Spread the love

BODI ya Maji Bonde la Rufiji (RBWB) imesema iwapo mvua zitanyesha kwa kipindi cha miaka miwili ya msimu, Bwawa la Mwalimu Nyerere litakalozalisha megawati 2,115 za umeme litakuwa limejaa maji. Anaripoti Selemani Msuya, Rufiji…(endelea).

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa RBWB, Mhandisi Florence Mahay wakati akizungumza na waandishi wa habari waliotembelea Mradi wa Kuzalisha Umeme wa Julius Nyerere (JNHPP) uliopo wilayani Rufiji mkoani Pwani.

Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), Profesa Japhet Kashaigile akieleza namna wanavyotafiti kuhusu upotevu wa maji kwenye vyanzo vya maji.

Mhandisi Mahay amesema Bonde la Rufiji lina maji futi za ujazo bilioni 40 ambapo maji juu ya ardhi futi za ujazo bilioni 31 na chini ya ardhi ni futi za ujazo bilioni 9, hivyo iwapo kutakuwa na usimamizi shirikishi katika vyanzo vya maji bwawa hilo litajaa ndani ya misimu miwili ya mvua.

Amesema Mto Rufiji ambao unaingizwa maji kwenye Bwawa la Nyerere unapokea maji kutoka katika mito mitatu mikubwa ambayo ni Kilombero inayochangia asilimia 65, Ruaha Mkuu asilimia 16 na Luwegu asilimia 19.

“Ili Bwawa la Nyerere lijae na kuweza kuzalisha umeme wa ukakika ni jukumu la RBWB kushirikiana na wadau mbalimbali ili vyanzo vya maji na mazingira viweze kuwa salama na endelevu.

Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Maji Bonde la Rufiji (RBWB), Mhandisi Florence Mahay akizungumza na waandishi wa habari namna wanasimamia bonde ili maji yaingie Bwawa la Nyerere

Mfumo wa maji Bonde la Rufiji unaweza kuzalisha maji futi za ujazo bilioni 40, futi za ujazo bilioni 31 yapo juu ya ardhi, hivyo hili Bwawa la Nyerere linahitaji futi za ujazo bilioni 30.6. Tunategemea ndani ya miaka miwili hadi mitatu bwawa litakuwa linajaa,” amesema.

Mkurugenzi huyo amesema katika kufanikisha Bwawa la Nyerere halikosi maji watahakikisha anayetumia maji ni yule ambaye ana kibali ambapo hada sasa wametoa vibali 2,005.

Aidha, amesisitiza kuwa katika mwaka wa fedha 2023/2024 wataajiri walinzi wa maji, ili kukabiliana na waharibifu wa vyanzo vya maji katika bonde hilo muhimu katika sekta ya nishani na kilimo nchini.

Kwa upande Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA), Profesa Japhet Kashaigile amesema katika kuhakikisha rasilimali maji inakuwa endelevu wamefanya utafiti ambapo wamebaini shughuli za kibinadamu ndio zinaathari vyanzo vya maji.

Amesema kutokana na shughuli hizo za kilimo wamebaini udongo na viatilifu vimekuwa vikiongezeka kwenye maji, hali ambayo inapaswa kuzuiwa kwa nguvu zote.

Prof. Kashaigile amesema ili kukabiliana na hali hiyo wameweza kupanda miti rafiki na mazingira zaidi ya 45,000 katika Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya na Wanging’ombe mkoani Njombe.

Mtafiti huyo ameshauri uhamasishaji wa kilimo rafiki, hasa cha kutumia makinga maji, ili kupunguza mmomonyoko na uingizaji wa viatilifu kwenye maji.

“Pia tunashauri wakulima walime mita 60 kutoka kwenye vyanzo vya maji, kwani bila kufanya hivyo dhamira ya Serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan ya kuzalisha umeme megawati 2,115 haitaweza kufikiwa,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Rais Samia awataka wahariri kufanya kazi bila uoga, upendeleo

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan amewataka wahariri wa vyombo...

Habari Mchanganyiko

STAMICO yasaini mkataba wa bilioni 55.2 kuchoronga miamba GGML

Spread the loveSHIRIKA la Madini la Taifa (STAMICO) limezidi kufanya vizuri katika...

Habari Mchanganyiko

NMB yatoa traksuti za Mwenge wa Uhuru Mtwara

Spread the loveBENKI ya NMB imetoa traksuti kwa mkoa wa Mtwara ambako...

Habari Mchanganyiko

Yara yaja na bima ya mazao kwa wakulima

Spread the love  WAKATI serikali ikiweka mikakati mbalimbali kuimarisha sekta ya kilimo...

error: Content is protected !!