June 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

BVR yageuzwa biashara

Waandikishaji wakiwa kwenye foleni wa BVR

Spread the love

UANDIKISHAJI wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwa mfumo wa kielektroniki (BVR), umechukua sura mpya kutokana na baadhi ya watu kuwauzia nafasi wengine katika vituo vya kujiandikishia. Anaandika Ferdinand Shayo … (endelea). 

‘Wafanyabiashara’ hayo wamekuwa wakiwahi nafsi mapema na kisha kuziuza kwa wale ambao wanashindwa kuwahi hasa pale foleni inapokuwa ndefu na hata wengine kulazimika kulala vituoni.

Wananchi wa Kata ya Sinoni jijini hapa Hussein Issa na Swalehe Ramadhani wameeleza kuwepo kwa baadhi ya vijana ambao tayari wameandikishwa lakini hufika tena kituoni hapo mapema na kushika nafasi za mbele na baadaye huwauzia watu wengine, mchezo huu umekithiri katika vituo vingi.

Issa amesema kuwa, nafasi moja huuzwa kati ya Sh. 10,000 hadi 15,000 kwa mtu mmoja na kwamba, hugombaniwa na watu wengi.

“Watu wamegeuza BVR kama biashara, wanashika nafasi na kuwauzia watu jambo ambalo linakwamisha zoezi. Watu wengi wasiokuwa na kitu cha kutoa wanakaa kwenye foleni kwa muda mrefu bila kuhudumiwa,” amesema Issa.

Polpodia Massawe ambaye ni Mkazi wa Esso amelalamikia tabia mfumo huo wa BVR kuwa bado haujaweza kukidhi idadi kubwa ya watu kwani imemlazimu kuacha shughuli za kujiingizia kipato na kupanga foleni kwa muda wa siku 4 bila mafanikio. 

Ameasema kuwa, watu wengine wamekuwa wakikesha na kulala vituoni hapo ili kuwahi nafasi ambapo ameitaka serikali iongeze nguvu hasa kwenye vituo vya mijini vyenye idadi kubwa ya watu.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Daudi Filex Ntibenda aliyetembelea kituo hicho, amekaripia vikali tabia ya watu kuuza nafasi maarufu kama ‘ploti’ kwani ni kinyume cha utaratibu. 

Ntibenda pia amewataka wanasiasa kutoingilia uandikishaji ambapo amehamasisha wananchi wajitokeze kwa wingi.

error: Content is protected !!