
Wananchi wakiwa kwneye foleni ya kujiandikisha vitambulisho vya kupigia kura kwa mfumo wa BVR
ZOEZI la Uandikishaji katika daftari la wapiga kura katika Mfumo wa Kielektroniki (BVR), limegeuka kuwa mateso kwa baadhi ya wazazi wenye watoto wadogo na kujikuta vituoni usiku wa manane kusubiria zoezi hilo. Anaandika Jimmy Mfuru … (endelea).
Uchunguzi uliofanywa na MwanaHalisi Online limebaini kuwa akinamama hao wamekuwa wakifika maeneo ya vituo kuanzia saa nane usiku huku wakiwa na watoto mgongoni wakipigwa na baridi.
Maeneo ambayo hali hiyo imebainika watoto hao wakiteseka na baridi ni maeneo yaVingunguti machinjioni,Tabata darajani,Liwiti na Yombo maeneo mengine huku akina mama hao wakilalamikia hali ya mateso kwa malaika hao.
Maria Kweka amesema amefika kituoni Tabata Darajani majiraya usiku saa nane ili hawezi kupanga foleni ili aweze kujiandikisha asubuhi yake ambamo katika zoezi hilo akina mama wenye watoto na wazee lakini mambo yamekuwa tofauti.
Zoezi hilo lilianza jijini Dar es Salaam julai 22 linatakiwa kumalizikia julai 31 huku wengi wakilalamikia uchache wa siku kwa kuwa zoezi hilo limekuwa likilegalega huku mashine hizo zikionekana kuzidiwa.
More Stories
Uholanzi, Uturuki ‘waingia’ vitani
Kuvunjwa kwa Jiji la Dar giza nene latanda
Ukomo wa urais uheshimiwe