July 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

BVR Dar, rushwa nje nje!

Wakazi wa Ubungo wakiwa kwenye foleni ya kujiandikisha vitambulisho vya kupiga kura kwa mfumo wa BVR

Spread the love

IKIWA ni siku ya tatu leo, tangu zoezi la la uandikishaji wa Daftari la upigaji kura kutumia mfumo mpya wa Kielektroniki (BVR) kuingia Jijini Dar es Salaam rushwa imeonyesha kutawala kwa baadhi ya vituo vya uandikishaji. Anaandika Sarafina Lidwino … (endelea).

Licha ya kuanza kwa zengwe tangu siku ya kwanza zoezi hili lilipoanza, kutokana na matatizo mengi kujitokeza katika vituo rushwa imewakosesha wananchi wengi haki zao za msingi.

Changamoto nyingine ambazo zilikuwa zimejitokeza sana kwa siku za kwanza zilikuwa ni pamoja na, ubovu wa mashine, kuchelewa kwa waandikishaji vituoni hapo pamoja na kutowapa kipaumbele makundi maalum.

Kutokana na matatizo hayo na mengine mengi, Gazeti la MwanaHalisi Online lilifunga safari na kutembelea baadhi ya vituo vya Wilaya ya Kinondoni na Ilala, na kuweza kubaini matatizo mengi likiwemo la rushwa.

Moja katia ya vituo vichache kati ya vingi ambavyo ambavyo vilitembelewa ni pamoja na kituo cha Kinondoni Biafra, Mkwajuni, Ilala Bungoni, Buguruni ambapo lilibainika tatizo kubwa la rushwa.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti kati ya wahanga hao ambao wamepoteza haki zao za msingi kutokana na kutokuwa na pesa za kuhonga, wameilalamikiwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), na kusema haikujipanga kwa zoezi hilo.

Akielezea mmoja kati yako, Mkazi wa Ilala Bungoni (hakutaka kutaja jina) ameelezea kuhusu rushwa inavyotendeka kituoni hapo na kusema, “kunawatu wenye pesa zao ambao wanakuja hapa hawakai foleni bali wanatoa tu pesa”

Amesema, “tukiwa kwenye foleni utashangaa tu mtu anaenda kule mbele anatoa hela kisha anapewa namba kwa hiyo wanawauzia namba za mbele ili kesho yake wapate kitambulisho mapema”.

Amesema, hali hiyo imekuwa kero kwa wananchi wa hali ya chini, ambapo muda mwingine hupelekea kutokea kwa fujo vituoni kutokana kwamba inakuwa ngumu kuona mtu akitumia mabavu kupata haki.

Naye mkazi wa Mkwajuni, Rebeka Salum ambaye alikuwa katika foleni ya kujiandikisha, alisema, “mbali na hilo la rushwa lakini pia lipo la kero ya matusi na lugha mbaya kutoka kwa hudumu wa vituo vingi.

Salumu amesema, inaonekana baadhi ya mawakala wengi hawakupatiwa elimui ya kutosha kuhusu uandikishaji kitu ambacho kinwapelekea mawakala wengi kugombana na waandikishwaji.

Akizungumzia tatizo la rushwa na lugha chafu zinazotolewa na mawakala hao leo Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiq amewataka wananchi wanaokubwa na matatizo hayo kutoa taarifa mapema sehemu husika.

Sadiq amesema, anashangwazwa sana na vitendo vinavyofanywa na mawakala hao kwani kabla ya kuanza kwa zoezi hili walipewa mafunzo ya kutosha.

“Mimi binafsi pia nimeshapata meseji nyingi kutoka kwa wananchi tofauti wakilalamikia matatizo haya, japo jana nilijaribu kutembelea katika baadhi ya vituo vya hapa Dar na sikuliona hilo tatizo la rushwa”.amesema.

Aidha,metoa wito kwa wananchi ambao wanakutwa na matatizo hao watoe taarifa kwa viongozi husika na wasikubali kutoa rushwa wanazodaiwa bali wawakamate na kuwafikisha sehemu husika.

error: Content is protected !!