
Waziri Mkuu Mstaafu, Jaji Joseph Warioba (kulia) akiteta jambo na Joseph Butiku
KESHO Jijini Dar es Salaam, moto utawashwa kupitia kongamano liloandaliwa na Taasisi ya Mwalimu Nyerere, ambamo Waziri Mkuu Mstaafu, Jaji Joseph Warioba na Mkurugenzi wa taasisi hiyo, Joseph Butiku watawasha moto kuhusiana uchaguzi mkuu wa uongozi wa awamu ya tano. Anaandika Pendo Omary … (endelea).
Katika taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari jioni hii (MwanaHALISI Online inayo) na Joseph Butiku, Mkurugenzi wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere inasema, “…ni kuhusu kongamano la amani na umoja kuelekea uchaguzi mkuu na uongozi wa awamu ya tano,”
Butiku amesema kongamano hilo litafanyika kesho saa 8.00 mchana hadi saa 11.00 jioni katika ukumbi wa Julius Nyerere (JNICC).
Mbali na ushiriki wa Butiku na Warioba wengine walioalikwa kwenye kongamano hilo,Profesa Palamagamba Kabudi,Profesa Mwesiga Baregu Ally Awadh na Humphrey Polepole waliokuwa wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba ambao watashiriki kutoa mada.
Taasisi ya Mwalimu Nyerere imejizolea umaarufu kwa kufanya utetezi wa maslahi mapana ya umma kwa kufuata misingi ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere.
Tarehe 19 Mei, mwaka huu taasisi hiyo iliendesha mkutano wa “kujadili amani, umoja na utulivu nchini” ambapo viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na serikali walikacha kuhudhuria.
More Stories
Uholanzi, Uturuki ‘waingia’ vitani
Kuvunjwa kwa Jiji la Dar giza nene latanda
Ukomo wa urais uheshimiwe