August 19, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Butiku ataka nguvu ielekezwe kwenye maendeleo ya wananchi kuliko vyama

Mrugenzi wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Mzee Joseph Butiku

Spread the love

 

MKURUGENZI wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Mzee Joseph Butiku, ameishauri Serikali na jamii, kujikita katika mipango ya maendeleo ya wananchi, badala ya kuelekeza nguvu kwenye siasa, ili kudumisha mfumo wa vyama vingi nchini. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Mzee Butiku ametoa maoni hayo leo Ijumaa, tarehe 1 Julai 2022, akitoa ujumbe wake kuhusu maadhimisho ya miaka 30 ya mfumo wa vyama vingi vya siasa, baada ya kuwasilisha mapendekezo yake juu ya uboreshaji wa demokrasia na mifumo ya sheria, katika Kikosi Kazi cha Rais, jijini Dar es Salaam.

“Tukijielekeza fikra, kauli na mawazo ya mipango yetu katika kuhudumia watu wetu, kuwawezesha waendelee kiuchumi, waelewe vizuri nchi yao kisiasa, watumie maisha na misingi yao kujenga umoja na amani yetu,” amesema Mzee Butiku.

Mzee Butiku amesema “tukienda na mambo ya wananchi tukaelekeza nguvu zetu huko kuliko nguvu kwenye vyama kinadharia, nadhani tutakwenda vizuri.”

Mwanasiasa huyo mkongwe nchini Tanzania, amesema Rais aliyeko madarakani, Samia Suluhu Hassan, anajitahidi katika kutekeleza masuala hayo.

error: Content is protected !!