May 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Butiku asema katiba mpya ni muhimu lakini…

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Joseph Butiku

Spread the love

 

MKURUGENZI Mtendaji na Mjumbe wa Bodi ya wadhamini wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Joseph Butiku amesema Katiba mpya na yenye mawazo ya wananchi ni muhimu japo Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan anataka kupewa muda. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Ametoa kauli hiyo wakati wa ufunguzi wa mdahalo leo Alhamisi tarehe 19 Agosti 2021 wa kubadilishana mawazo ili kuimarisha maarifa, taaluma, ujuzi na weledi kuhusu wajibu wa pamoja wa wadau wa kisiasa katika kujenga na kusimamia utekelezani wa Msingi ya Mfumo wa Demokrasia ya vyama vingi nchini Tanzania.

Amesema takwa la katiba ni muhimu kwani nchi haijawahi kuwa na katiba mpya licha ya kuwa iliyopo imekuwa ikiwekewa viraka.

“Takwa la katiba ni muhimu kwani tumekuwa tukidai katiba kwa muda mrefu na iliyopo imekuwa imiwekwa viraka. Mimi namshukuru Mungu kwani katika tume ya kukusanya maoni nilikuwepo na tulikusanya maoni ya wananchi na likaitishwa Bunge la Katiba na kuwepo kwa katiba pendekezwa,” amesema

“Lakini kwa sasa tumepata Rais mpya ambaye pia anakubaliana na Katiba mpya ila amekuwa akisisitiza kupewa muda wa kuweza kushughulikia suala la katiba Mpya” amesema Butiku.

Rais Samia aliyeingia madarakanbi tarehe 19 Machi 2021 baada ya kifo cha aliyekuwa Rais John Pombe Magufuli, amesema takwa la katiba mpya analifahamu lakini amewaomba Watanzania kumpa muda ili aupandishe kwanza uchumi wa nchi.

Hayati Magufuli alifikwa n amauti saa 12 jioni ya tarehe 17 Machi 2021 katika Hospitali ya Mzena, iliyopo Makumbusho mkoani Dar es Salaam na mwili wake kuzikwa nyumbani kwao Chato Mkoa wa Geita.

Naye mhadhili wa Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo, Adam Msondo amesema taifa lina ombwe la uongozi kwa kukosa viongozi wenye maadili mema kwa kukosa namna ya kuwapata viongozi.

Hata hivyo, amesema ili serikali ya demokrasia ya kweli ni lazima kuwa viongozi ambao wanajitambua.

Kuhusu demokrasia ya kweli amesema, tunahitaji kuwa na demokrasia ya kwetu bila kutafuta demokrasia kutoka katika sehemu nyingine ambayo itamuwa na Maridhiano.

Naye Aisha Madoga ambaye ni Mwenyekiti wa baraza la wanawake Chadema (BAWACHA) Mkoa wa Dodoma amesema, pamoja na kuwa na wimbo wa demokrasia lakini bado hakuna uhalisia.

“Imekuwa ikishangaza kuona ni namna gani ambavyo Watanzania wanavyozuiliwa hata kumkosoa rais pale ambapo anakosea.”

“Lakini hata ukiangalia jinsi walivyopatikana wawakilishi wa wananchi utabaini kilichofanyika ni kuwapora watu ushindi wao,” amesema.

error: Content is protected !!