July 1, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Burkina Faso: Viongozi wa jeshi wagombania nafasi ya kutawala nchi

Spread the love

Mgawanyiko umetokea kati ya makamanda wa jeshi juu ya nani anaongoza nchi kufuatia kujiuzulu kwa Rais Blaise Compaore aliyekuwa madarakani kwa miaka 27 kufuatia shinikizo la maandamano na fujo zilizofanywa na wananchi.

Mlinzi msaidizi wa aliyekuwa Rais wa Burkina Faso Rais Kanali Isaac Zida amesema yeye ndiye mkuu wanchi aliyeshikilia nchi katika kipindi hiki cha mpito. Mwanzoni Mkuu wa majeshi Jenerali Honore Traore alisema ndiye aliyeshikilia madaraka kwa kipindi hiki.

Akiongea siku ya jumamosi Kanali Zida alisema madai ya Jenerali Traore kuwa ndio kiongozi wanchi sio kweli. “Kwa sasa mimi ndio mkuu wa nchi na ninawajibika na utekelezaji wa kipindi cha mpito kuhakikisha nchi inaendelea na uwepo wa demokrasia” alisema Kanali Zida wakati akifanya mahojiano na Televisheni ya ZFP.

Wakati huo huo Kanali Zida alisikika kwenye radio akisema kuwa yeye ndio mkuu wa nchi na kuzitaka nchi za Afrikana taasisi za Ushirikiano wa Kikanda kama vile Ecowas kuunga mkono uongozi huo wa mpito.

Sintofahamu hii imekuja baada ya waandamanaji wa Burkina Faso kukasirishwa na mpango wa serikali kupitia Bunge la nchi hiyo kupeleka mswada Bungeni ili kuongeza muda wa urais kuwepo madarakani, kitendo kilichopelekea wananchi hao wenye hasira kuvamia ukumbi wa bunge na kuuchoma moto.

Siku ya Ijumaa Mr. Campaore alitoa maelezo kuwa amejiudhuru na nafasi ya urais ipo wazi, huku akishawishi uchaguzi ufanyike ndani ya siku 90. Hata hivyo haijajulika kwa sasa yupo wapi.

error: Content is protected !!