August 10, 2022

Uhuru hauna Mipaka

‘Buriani Thomas Mashali’

Mwili wa Thomas Mashali ukizikwa katika makaburi ya Kinondoni

Spread the love

THOMAS Mashali, aliyekuwa bondia mashuhuri nchini Tanzania, amezikwa leo kwenye makaburi ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam, anaandika Faki Sosi.

Mashabiki, wapenzi wa ndondi, wananchi na wanafamilia kwa pamoja leo wauaga mwili wa Mashali katika Ukumbi wa Diamon Jubilee kabla ya kwenda kuuzika Kinondoni.

Awali Mashali alitarajiwa kuzikwa jana lakini baadaye familia yake iliahirisha maziko hayo na kufanyika leo.

error: Content is protected !!