January 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Bungo ahimiza wananchi kuchagua Ukawa

Spread the love

MGOMBEA ubunge wa Jimbo la Mbagala kupitia CUF, Kondo Bungo amehamasisha wakazi wa jimbo hilo kumchagua yeye pamoja na madiwani wa waliopitishwa na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa). Anaandika Faki Sosi … (endelea).

Katika mahujiano yake na MwanaHALISI Online yaliyofanyika leo kwa njia ya simu, Bungo amesema kuwa, anaendelea na ziara ya kuhamasisha wananchi wa jimbo hilo kuchagua Ukawa katika ngazi zote.

Wakati akizungumza na mwandishi alikuwa tayari ametembelea kata nne za Kijichi, Mbagala Kuu, Kiburugwa na Mbagala.

“Madiwani ndio kiunganishi kikubwa cha kuiletea maendeleo Mbagala kutokana na kuwa na lengo moja kwa wananchi,” amesema Bungo.

Madiwani hao ni Ramadhani Kambangwa wa Kata ya Mbagala, Khalidi Shamaki wa Kata ya Kijichi, Mashaka wa Kata ya Mbagala Kuu na Mustafa Ismail wa Kata ya Kiburugwa.

“Wapiga kura wa Mbagala wanahitaji mabadiliko hivyo basi ni lazima kupata viongozi wanaotoka kwenye kambi ya wanamabadiliko ambayo ni Ukawa ili kurahisisha kazi ya kuleta mabadiliko ya kweli katika jimbo,” amesema Bungo.

Bungo ameipa angalizo Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na serikali kutoenda kinyume na maadili na sheria zilizowekwa ili kulinda amani ya nchi.

Bungo ametuhumu wafuasi wa CCM kwa kuchana mabango yake ya kampeni katika mitaa mbalimbali kwenye jimbo hilo.

error: Content is protected !!