Tuesday , 5 December 2023
Home Habari Mchanganyiko Bunge yaitaka TASAF kuongeza kwenye ajira
Habari Mchanganyiko

Bunge yaitaka TASAF kuongeza kwenye ajira

Mwanne Nchemba, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala bora na Serikali za Mitaa
Spread the love

MWENYEKITI wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala Bora na Serikali za Mitaa, Mwanne Nchemba ameushauri Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) kuongeza nguvu kwenye utoaji wa ajira kwa vijana kwenye kaya maskini kupitia miradi ya TASAF III, anaandika Christina Haule.

Mwanne amesema hayo wakati kamati hiyo ilipotembelea miradi mbalimbali ya TASAF ikiwemo ya ugawaji fedha za uhawilishaji katika mitaa wa Kilongo kata ya Mkundi Manispaa ya Morogoro.

“Ikiwa vijana wa kutoka kwenye familia maskini watapatiwa ajira zinazotokana na miradi ya TASAF wanaweza kupata fedha za kujikimu wao pamoja na wategemezi wao, na hivyo kutimiza lengo la TASAF la kusaidia kaya maskini,” amesema Mwanne.

Awali Mkurugenzi anayesimamia programu za jamii wa TASAF, Amades Kamagenge amesema, TASAF kwa sasa inaendelea na zoezi la uhawilishaji wa fedha kwa kaya maskini zinazokula mlo mmoja na baadae watajikita kwenye miradi.

Kamagenge amesema, miradi huwainua walengwa kwa kujikwamua na uchumi ambapo mpaka sasa Halmashauri 161 zimeingizwa katika miradi ya TASAF.

Aidha alizitaka halmashauri zilizoziondoa kaya zilizodaiwa kuwa siyo maskini na kugundua kuwa ni maskini baada ya kujiridhisha, kutibitisha jambo hilo kimaandishi na kisha kupeleka maombi ili yaweze kufanyiwa kazi.

Naye Mwenyekiti wa mtaa wa Kilongo, Thabit Makanyaga aliipongeza TASAF kwa mpango wake wa uhawilishaji wa fedha kwa kaya maskini kwani hadi sasa tayari kaya 16 zimenufaika na biashara zao baada ya kuwezeshwa na mpango huo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

RPC Songwe awafunda trafki kuzingatia uadilifu

Spread the loveASKARI wa kikosi cha usalama barabarani mkoani Songwe wametakiwa kuendelea...

Habari Mchanganyiko

Mchimba madini jela maisha kwa kubaka, alihonga Sh 500

Spread the loveMahakama ya wilaya ya Songwe imemtia hatiani na kumhukumu kifungo...

Habari Mchanganyiko

Mlima wa Moto wazindua kongamano la SHILO kumuenzi Rwakatare

Spread the loveKANISA la Mlima wa Moto Mikocheni jijini Dar es Salaam,...

Habari MchanganyikoTangulizi

20 wafariki dunia kwa mafuriko Manyara

Spread the loveMVUA za vuli zinazoendelea kunyesha maeneo mbalimbali nchini zimeleta madhara...

error: Content is protected !!