Friday , 19 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Bunge: Serikali ifanye tathimini maombi ahirisho la madeni
Habari za Siasa

Bunge: Serikali ifanye tathimini maombi ahirisho la madeni

Spread the love

 

SERIKALI imeshauriwa kufanya tathimini ya kina kabla ya kuomba ahirisho la kulipa madeni ya Serikali. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Serikali ipo kwenye mazungumzo na nchi wanachama wa Paris (Paris Club) na wasio wanachama na zile zilizoikopesha kwa njia ya billateral ili kuangalia namna ya kuahirisha ulipaji wa madeni katika kipindi hiki ambacho hali ya ukuaji wa uchumi umeathiriwa na janga la Uviko-19 na vita vya Urusi na Ukrenia.

Akisoma taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, leo Jumanne tarehe 7 Juni, 2022, Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Omary Kigua, amesema jambo hilo lina mitazamo miwili.

Amesema mtazamo wa kwanza ni kuwa hatua hii itatoa ahueni kwenye bajeti na kuiwezesha Serikali kufanya miradi mingine huku upande mwingine ikiwa ni edapo Serikali itakua na mapato ya kutosha kulipa pindi madeni hayo yatakapoiva.

“Muda wa kulipa ukifika lazima mapato yawepo na uwezo wa kubeba madeni yaliyoiva ya wakati huo na yaliyoahirishwa,” amesema na kuongeza;

“Lazima Serikali ifanye tathimini ya kina na kuangalia endapo mapato yataweza kubeba mzigo huo kabla ya kuomba ahirisho.”

Ameongeza pia kuwa Serikali itafute namna itakavyoweza kuongeza mapato ya fedha za kigeni ili deni la Serikali kuendelea kuwa himilivu, “mfano kutumia vyanzo bunifu vya fedha kama infrastructure bond, carbon credit.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Tanzania, Uturuki zanuia kukuza biashara, uwekezaji

Spread the loveSERIKALI za Tanzania na Uturuki zimekubaliana kuendeleza dhamira ya kuimarisha...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza ajira watendaji daftari wapiga kura

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), imetangaza nafasi...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema yatangaza ruti awamu ya pili maandamano

Spread the love  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema awamu ya...

Habari za Siasa

CCM yamkana mwenyekiti UVCCM aliyetaka wapinzani wapotezwe

Spread the love  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimejitenga na kauli ya mwenyekiti...

error: Content is protected !!