Thursday , 28 March 2024
Habari za Siasa

Bunge Live larejea

Spread the love

VIKAO vya Bunge la Tanzania vitaanza kurushwa mubashara kuanzia kesho Jumanne, tarehe 5 Aprili 2022. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma…(endelea).

Taarufa hiyo imetolewa leo Jumatatu, tarehe 4 Aprili 2022, jijini Dodoma na Katibu wa Bunge, Nenelwa Mwihambi, akitoa ratiba ya Mkutano wa Saba wa Bunge unaoanza kesho.

Mwihambi amesema vikao hivyo vitaanza kurushwa mbashara baada ya Kamati ya Uongozi ya Bunge, kuridhia kufuatia kukamilika kwa maboresho ya studio ya mhimili huo.

Katibu huyo wa Bunge, ameviomba vyombo vya habari kutenga muda kwa ajili ya kurusha vikao hivyo.

“Vituo vya redio, chaneli za Tv na mitandao ya kijamii, wanaotaka watachukua matangazo hayo kutoka kwenye studio zetu moja kwa moja. Lakini naomba muujulishe umma na wenye vyombo vya habari wapokee hilo jambo na watutengee muda kwenye vituo vyao moja kwa moja,” amesema Mwihambi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

error: Content is protected !!