Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Bunge lisiwe ndumilakuwili – Kubenea
Habari za Siasa

Bunge lisiwe ndumilakuwili – Kubenea

Bunge likiendelea na vikao vyake
Spread the love

MBUNGE wa Ubungo, Saed Kubenea, amehoji uhalali wa Bunge kuwaadhibu wabunge wa upinzani na “kuwanyamazia” wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), anaandika Erasto Masalu.

Akizungumza bungeni leo asubuhi (Ijumaa), Kubenea amesema, kumejengeka utaratibu mbaya ndani ya Bunge hili wa kuwapendelea wabunge wa CCM na kuwanyonga wabunge wa upinzani.

Kubenea alitoa mfano wa Mbunge wa Viti Maalum, Lucy Mayenga aliyedai kuwa wabunge wanaozungunzia vitendo vya utekaji na utesaji bungeni, wanatoa kauli hizo kwa kuwa wamehongwa.

Amesema, “…naibu Spika, wakati Mheahimiwa Lucy Mayenga anazungumza bungeni alidai kuwa wabunge wanaozungumzia utekaji wamehongwa. Nilipomtaka athibitishe au afute kauli yake, mwenyekiti alidai hakusikia.

“Akaahidi kusoma Hansard (kumbukumbu za Bunge), lakini mpaka leo hajatoa majibu. Lakini hata pale lipoendelea kuchangia, bado alisistiza kuwa ana ushahidi wa anachokisema.”

Amesema, kinyume na inavyokuwa kwa wabunge wa upinzani, kwamba hata pale ambapo wanafanya makosa madogo, huchukuliwa hatua, lakini wabunge wa CCM wanalindwa.
Kubenea alilitaka Bunge kutokuwa “ndumilakuwili” bali lisimame kwenye haki.

Akijibu muongozo huo, Naibu Spika, Tulia Ackson alimtaka Kubenea kufuatilia suala hilo kwenye utawala kwa kuwa ndani ya kanuni za Bunge, hakuna ukomo wa siku ya kutolewa hukumu.

Naye Kubenea akizungumza na MwanaHALISI Online kwa njia ya simu kutoka Dodoma, aliahidi kufuatilia suala hilo hadi kuhakikisha haki inatendeka.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Chadema yamtaka Rais Samia aunde tume kuchunguza mauaji mgodi wa Barick

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, ameombwa aunde tume huru kwa...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

error: Content is protected !!