Monday , 4 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Bunge latoa siku saba serikali kutoa takwimu za watumishi
Habari za Siasa

Bunge latoa siku saba serikali kutoa takwimu za watumishi

Spread the love

SPIKA Job Ndugai ametoa siku saba kwa Wizara ya Ofisi ya Rais-TAMISEMI kutoa takwimu za watumishi wake waliopandishwa madaraja, walioajiriwa katika mwaka wa fedha wa 2012/13. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Ndugai ametoa agizo hilo baada ya kutoridhishwa na majibu ya Naibu Waziri Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Josephat Kandege kuhusu malalamiko ya baadhi ya watumishi walioajiriwa mwaka wa fedha wa 2012/13, kutopandishwa madaraja hadi leo.

Amesema wizara hiyo itakapoleta takwimu hizo itasaidia kujua tatizo la watumishi kutopandishwa madaraja liko kiasi gani, huku akieleza kwamba uzembe wa maafisa watumishi ni miongoni mwa sababu za changamoto hiyo.

Ndugai amesema kuwa, swali hilo litaulizwa tena bungeni Alhamisi ijayo tarehe 15 Novemba 2018 pindi takwimu hizo zitakapoletwa bungeni.

Awali, Kandege alijibu kuwa, kutokana na sababu mbalimbali baadhi ya watumishi walioajiriwa katika mwaka huo wa fedha hawajapandishwa madaraja, na kubainisha kwamba watumishi waliokuwa na sifa stahiki na kujaza fomu inavyotakiwa walipandishwa madaraja.

“Ni kweli kuna wakati walioajiriwa pamoja walistahili kupanda kwa pamoja, kuna wakati hawapandi kwa pamoja kutokana na sababu tofauti, hali ya kawaida kama sifa zote zinalingana na kujaza fomu inavyotakiwa serikali haimuachi mtu sababu wanapopandishwa serikali haipendelei,” amejibu Kandege.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Dk. Mwinyi aungana na Samia kuuaga mwili wa baba yake

Spread the loveRais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk....

Habari za SiasaTangulizi

Mtoto wa Mzee Mwinyi amwaga machozi

Spread the loveMtoto wa Hayati mzee Mwinyi, Abdullah Ali Hassan Mwinyi ameshindwa...

Habari za SiasaTangulizi

Mzee mwinyi alikuwa mwanademokrasia wa kweli

Spread the loveMtoto wa Hayati Ali Hassan Mwinyi, Abdullah Ali Hassan Mwinyi...

Habari za SiasaTangulizi

Samia: Mwinyi alikuwa maktaba inayotembea

Spread the loveRais Samia Suluhu hassan amesema Hayati rais mstaafu, Ali Hassan...

error: Content is protected !!