May 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Bunge latengua kanuni

Bunge la Tanzania

Spread the love

 

BUNGE la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, limetengua kanuni kanuni ya 160 (1) ili kuruhusu wasio wabunge kuingia ukumbini. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma…(endelea).

Kanuni hiyo imetenguliwa leo Alhamisi tarehe 22 Aprili 2021, baada ya Jenista Muhagama, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Wenye Ulemavu kutoa hoja ya utenguzi wa kanuni hiyo.

Hoja hiyo imeungwa mkono na wabunge baada ya kuhojiwa na Spika wa Bunge, Job Ndugai kutokana na ujio wa Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kuhutubia Bunge kwa mara ya kwanza.

Utenguzi wa kanuni hiyo, sasa unaruhusu mtu asiyekuwa mbunge kuingia katika ukumbi wa bunge, Rais Samia pamoja na viongozi wengine wa ngazi za juu nchini, wataingia ndani ya ukumbi huo.

Mbali na Rais Samia, viongozi wengine watakaoingia ndani ya ukumbi wa bunge ni pamoja na Rais wa Zanzibar, Dk. Hussein Mwinyi; Makamu wa Rais Tanzania, Dk. Philip Mpango; Makamu wa Kwanza na wa Pili wa Rais Zanzibar; Jaji Mkuu wa Tanzania; Jaji Mkuu wa Zanzibar; Spika wa Bunge la Afrika Mashariki na Spika wa Baraza la Wawakilishi.

error: Content is protected !!