Thursday , 25 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Bunge lataka waliohusika na upotevu wa Bil. 8 Bandari washughulikiwe
Habari za Siasa

Bunge lataka waliohusika na upotevu wa Bil. 8 Bandari washughulikiwe

Sehemu ya magari yakiwa bandarini yakisubiri kutolewa na wamiliki wake
Spread the love

 

KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) imeitaka Serikali ichukue hatua dhidi ya kampuni na watendaji wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), walioisababishia mamlaka hiyo hasara ya Sh. 3.23 bilioni na dola za Marekani 2.30 milioni (Sh. 5.33 bilioni), katika kipindi cha miaka 10 (2010 hadi 2020).Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Hasara hiyo inadaiwa kutokana na kutokukamilika kwa usimikaji mfumo wa kielektroniki wa TPA wa Upangaji Rasilimali za Biashara (ERP).

Wito huo ulitolewa jana Alhamisi, tarehe 17 Februari 2022 na Mwenyekiti wa PAC, Naghenjwa Kaboyoka, bungeni jijini Dodoma.

Akisoma taarifa ya kamati hiyo, kuhusu taarifa za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG), kwa hesabu zilizokaguliwa za Serikali Kuu na mashirika ya umma, kwa mwaka wa fedha ulioshia tarehe 30 Juni 2020.

“Serikali ichukue hatua za kisheria kwa Kampuni zote ambazo zimehusika kuisababishia TPA hasara, kama zilivyobainishwa kwa kina katika taarifa ya ukaguzi maalumu wa kiuchunguzi wa mfumo wa ERP, uliofanywa na CAG,” amesema Kaboyoka.

Kaboyoka amesema “watumishi wote wa TPA waliotajwa kushiriki mchakato wa manunuzi na usimikaji wa mfumo wa ERP, wachukuliwe hatua kwa kuzingatia matokeo ya kiuchunguzi na uhusika wa kila mmoja katika mchakato huo.”

Wakati huo huo, Kaboyoka ameitaka Serikali itumie taasisi ya umma ya Wakala wa Serikali Mtandao (E-Government), katika kusimamia na kuratibu shughuli zinazoendelea za uwekaji mifumo ya TPA.

“Jambo hili litasaidia kuongeza uwajibikaji na kupunguza gharama , ambazo Serikali imekwishaingia hadi sasa,” amesema Kaboyoka.

Akisoma taarifa ya PAC kuhusu matokeo ya chunguzi wa CAG, juu ya mfumo huo, Kaboyoka amesema, mfumo wa ERP ulitakiwa kutekelezwa kwa awamu nne,.

Kaboyoka amedai , chanzo cha hasara hiyo ni TPA kutofuata mwongozo wa kuishirikisha Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA), katika maandalizi ya utekelezaji wa mifumo.

Kinyume na matakwa ya kifungu 4.2.1, cha mwongozo wa matumizi bora wa vifaa vya teknolojia ya habari na mawasiliano Serikalini (TEHAMA).

“Hali kadhalika, ukaguzi ulibaini TPA ilikuwa imesimika mifumo zaidi ya kumi (10), ambayo haikuwa inasomana , hivyo kutokuwa na tija na ufanisi kwa Shirika,” amesema Kaboyoka.

Mwenyekiti huyo wa PAC amedai, ukaguzi wa CAG umebaini TPA ilitoa tuzo ya mkataba wa kusimika mfumo huo awamu ya kwanza, kwa Kampuni ya Soft Tech Consultant Limited (STCL), kwa gharama ya Sh. 694,142,960, ambayo haikuwa na sifa na uwezo stahili.

“STCL ililipwa kiasi cha Sh. 600,433,963 sawa na asilimia 87 ya mkataba pamoja na mkataba husika kusitishwa, hivyo TPA ilipata hasara ya Sh. 600,433,963,” amedai Kaboyoka.

Mwenyekjiti huyo wa PAC amedai “TPA iliingia mkataba wa nyongeza na STCL wa Dola za Kimarekani 31,860 kwa ajili ya mafunzo ya watumishi 165 licha ya mkataba wa awali kuhusisha mafunzo ya aina ileile.”

Kaboyoka amedai, ukaguzi wa CAG umebaini kiasi cha Sh. 12,177,480, kililipwa isivyostahili kutokana na kubadilishwa sifa za vifaa vilivyopangwa kufungwa kwenye mradi.

“Ukaguzi ulibaini pia, Kampuni ya Twenty Third Century Systems (TTCS), ilipewa tuzo ya mkataba Na. AE/016/2014-15/CTB/G/39 , wa Dola za Kimarekani 6,635,387.16, kwa upendeleo kwa kuwa haikuwa na sifa stahiki,”
“Mkataba huu pia ulivunjwa wakati TPA akiwa amelipa kiasi cha Dola za Kimarekani 4,632,099 sawa na asilimia 70 ya thamani ya mkataba wakati utekelezaji ukiwa kwa asilimia 42,” amedai Kaboyoka.

Aidha, Kaboyoka amedai, ukaguzi wa CAG umebaini, TPA ilipata hasara ya kiasi cha Dola 433,011, kwa kuingia mkataba wa ziada na Kampuni ya SAP – East Africa Ltd, ili kuhakiki kazi zilizotekelezwa kwenye mkataba uliovunjwa wa Kampuni ya TTCS.

“Fedha hizo zingeokolewa endapo mkataba wa TTCS, ungetekelezwa ipasavyo. Ukaguzi ulibaini udanganyifu katika upekuzi wa mikataba, hali iliyosababisha masharti mapya kujumuishwa kwenye mikataba wakati hayakuwa sehemu ya nyaraka ya zabuni,” amedai Kaboyokwa na kuongeza:

“ Mwisho ukaguzi ulibaini kuwa, mikataba miwili kati ya TPA na SAP – East Africa Ltd, yenye thamani ya Dola 433,011 na Dola 997,647 mtawalia, haikuwasilishwa kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, kwa ajili ya upekuzi. Suala hili ni kinyume na masharti ya Kanuni ya 59(2)(1)(b) ya Kanuni za Ununuzi wa Umma za Mwaka 2016.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

error: Content is protected !!