Spread the love

 

BUNGE la Tanzania, limeitaka Serikali litoe taarifa za matumizi ya asilimia 10 za mapato ya ndani ya halmashauri, zilizotolewa kwa ajili ya mikopo kwa wananchi kuanzia 2018 hadi 2022. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Agizo hilo limetolewa leo Alhamisi, bungeni jijini Dodoma na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa, Dennis Londo, akiwasalisha taarifa ya kamati hiyo kuhusu utekelezaji majukumu ya Ofisi ya Rais-TAMISEMI.

“ Serikali iandae taarifa maalum ya matumizi ya fedha za asilimia 10, inayotokana na mapato ya ndani ya Halmashauri zinazotokana na mapato yasiyolindwa,”

“ Taarifa hizo zioneshe kiasi kilichokusanywa tangu mwaka 2018 hadi 2022, kiasi kilichokopeshwa, kiasi kilichorejeshwa, kiasi kilichotumika kwa usimamizi pamoja na fedha za marejesho kwa kila Halmashauri,” amesema Londo.

Waziri wa Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Innocent Bashungwa

Aidha, Londo ameishauri Serikali iweke utaratibu wa ufuatiliaji na usimamizi wa fedha hizo, ili yawe na tija.

“Matumizi ya fedha za asilimia 10 inayotokana na mapato ya ndani ya Halmashauri yasipowekewa utaratibu mzuri wa ufuatiliaji na usimamizi, hayatatoa tija iliyokusudiwa. Kwa sasa, taarifa za matumizi ya fedha hizo zinatofautiana kwa kiasi cha kuacha mashaka kuhusu uaminifu katika matumizi yake,” amesema Londo.

Katika hatua nyingine, Londo ameishauri Idara ya Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii na Biashara za halmashauri, zitumike katka kuviwezesha vikundi vinavyopata mikopo, ili vifanye biashara kwa ufanisi na viweze kurejesha fedha vinazokopa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *