July 6, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Bunge lampoteza Mwaiposa wa Ukonga

Marehemu, Eugen Mwaiposa (55)-aliye Mbunge wa Ukonga 2010-2015 enzi wa uhai wake

Spread the love

EUGEN Mwaiposa (55)-aliye Mbunge wa Ukonga 2010-2015, amefariki dunia ghafla nyumbani kwake mjini Dodoma, ambapo yupo kwa ajili ya shughuli za Bunge la Bajeti linaloendelea.

Mwaiposa ni mbunge wa pili wa CCM kufariki dunia kwa ghafla mwaka huu, akitanguliwa na Mbunge wa Mbinga Magharibi, Kapteni John Komba.

Kwa mujibu wa taarifa fupi ya Bunge, Mwaiposa alikuwa na tatizo la shinikizo la damu kwa muda mrefu na amefariki nyumbani kwake eneo la Chaduru mkabala na jengo jipya la hoteli ya Shabiby barabara ya Dar es Salaam. Mwili wake umepelekwa hospitali ya mkoa wa Dodoma kwa uchunguzi zaidi.

Shughuli ya kuaga mwili wa marehemu itafanyika kesho baada ya familia yake kuwasili Dodoma. Bunge limesema litaendelea kuwajulisha wabunge kukiwa na taarifa zaidi.

“Kwa jinsi hiyo, natumia kanuni ya 152 kuahirisha Bunge hadi kesho kutwa (Alhamis),”amesema Naibu Spika katika taarifa yake.

Mwaiposa amezaliwa 23 November 1960 na kusoma Shule ya Msingi Nkweseto kati ya mwaka 1967 hadi 1974 kisha kujiunga na Sekondari ya Masama mwaka 1976 hadi 1980. Amepata elimu ya kidato cha tano na sita mwaka 1981 hadi 1983 katika shule ya Biashara Shinyanga.

Alijiendeleza zaidi kati ya mwaka 1986 hadi 1992 kwa kutunukiwa shahada ya uzamili katika Chuo cha Higher Economics Instute “Karl Marx”, Sofia, Bulgaria, 2004 hadi 2007 alisomea shahada nyingine ya uzamili katika Chuo cha Strathclyde, Glasgow.

Mwaiposa aliendelea na elimu ambapo mwaka 2006 hadi 2009, alitunukiwa cheti katika taasisi ya Hanns Seidel Foundation na mwaka 2007, alitunukiwa cheti katika Taasisi ya Eastern & Southern African Management Institute (ESAMI)

error: Content is protected !!