
Prof. Mussa Assad, Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) akiwa mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Haki, Maadili, Hadhi na Madaraka ya Bunge
PROF. Mussa Assad, mkaguzi na mdhibiti mkuu wa hesabu za serikali (CAG), amemaliza kuhojiwa na Kamati ya Haki, Kinga, Maadili na Madaraka ya Bunge. Mahojiano yalichukua takribani saa nne. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).
Prof. Assaad aliingia ndani ya Kamati hiyo, saa 4:47 asubuhi. Alitoka saa 8:48 mchana.
Haikuweza kufahamika mara moja, nini kilijadiliwa katika kikao hicho.
MwanaHALISI Online lilipomuuliza Prof. Asaad juu ya kilichojadiliwa, haraka alisema, “hapana. Sina la kusema.”Prof. Assad amekuwa kwenye mvutano na Bunge, mara baada ya kunukuliwa akiwa nchini Marekani akisema, hatua ya mhimili huo wa kutunda sheria na kusimamia serikali, kushindwa kufanyia kazi ripoti za ukaguzi za fedhaoinazoibuliwa na ofisi yeke, “ni sawa na udhaifu.”
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge, Emmanuel Mwakasaka amesema mahojiano na CAG yalienda vizuri.
More Stories
Dk. Mwinyi amteua Dk. Mkuya, Nassor Mazrui
Waziri Majaliwa aitaka TPA kuongeza umakini
Mrithi wa Maalim Seif ataja ‘kilichombeba’