Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Bunge lalia msongamano wa mizigo bandari Dar es Salaam
Habari za SiasaTangulizi

Bunge lalia msongamano wa mizigo bandari Dar es Salaam

Mwenyekiti wa Kamati ya PIC, Jerry Silaa
Spread the love

 

KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC),limeishauri Serikali kuchukua hatua za kumaliza changamoto za msongamano wa shehena za mizigo katika Bandari ya Dar es Salaam, inayopelekea kukosa mapato ya forodha. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Akiwasilisha taarifa ya mwaka ya shughuli za PIC, kuanzia Februari 2022 hadi Januari 2023, leo Jumanne, Mwenyekiti wa kamati hiyo, Jerry Silaa, amesema msongamano wa shehena za mizigo unaifanya Bandari ya Dar es Salaam, ishindwe kushindana na Bandari ya Mombasa nchini Kenya na Bandari ya Beira nchini Msumbiji.

“Kumekuwa na changamoto ya msongamano wa shehena za mizigo, kuongezeka kwa gharama za uendeshaji wa Bandari na kukosekana kwa mapato ya forodha kwani wanashindwa kushusha baadhi ya shehena za mizigo, katika Bandari ya Dar Es Salaam,”

“Changamoto hizi zinaisababishia Bandari ya Dar es Salaam kushindwa kushindana na Bandari za karibu yake ikiwemo Bandari ya Mombasa, Kenya na bandari ya Beira iliyopo nchini Msumbiji,” amesema Silaa.

Silaa amesema, licha ya upanuzi wa bandari hiyo unaonedelea hivi sasa, hautaweza kumaliza changamoto iliyokuwepo ya wingi wa shehena zinazohudumiwa na nyingine kushinfwa kushushwa kutokana na eneo kuwa dogo na kina kidogo.

Silaa amesema PIC inaishauri Serikali kupitia TPA, imalize changamoto zinazouzia kuanza kufanya kazi kwa Bandari Kavu ya Kwala, ambayo imekamilika kwa asilimia 98.

Pia, amesema PIC inaishauri Serikali kuharakisha mchakato wa ujenzi wa Bandari ya Mbegani-Bagamoyo kwa kutumia mapato ya ndani.

Silaa amesema PIC inaipongeza Serikali kwa kuteua Bodi Mpya ya Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) na kufanya mabadiliko katika menejimenti yake, kwa ajili ya kuongeza ufanisi wa mamlaka hiyo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

error: Content is protected !!