July 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Bunge lakwepa kufafanua madai mshahara wa Lissu

Steven Kigaigai, Katibu wa Bunge (kushoto). Picha ndogo Tundu Lissu

Spread the love

MADAI ya Tundu Lissu, Mbunge wa Singida Mashariki kwamba, amesitishiwa mshahara na stahili zake zingine za kibunge yameshindwa kupatiwa ufafanuzi. Anaripoti Regina Mkonde…(endelea).

Madai hayo yaliyotolewa jana na kusambazwa kwenye mitandao ya kijaami yameeleza kuwa, Ofisi ya Bunge imesitisha stahiki hizo kuanzia Januari mwaka huu na kwamba, hatua hiyo ni kinyume na utaratibu wa sheria.

MwanaHALISI ONLINE limemtafuta Steven Kagaigai, Katibu wa Bunge la Jamhuri ili kupata ufafanuzi kuhusu malalamiko ya Lissu ambaye ni Mnadhimu Mkuu wa Kambi ya Rasmi ya Upinzani bungeni, hata hivyo amegoma kufafanua. Mazungumzo yalikuwa hivi;

Mwandishi: Kuna malalamiko ya Lissu kwamba mshahara wake umezuiliwa tangu mwezi Januari, je taarifa hizi zina usahihi kwa namna gani?

Kagaigai: Malalamiko hayo sijayapata.

Mwandishi: Je, ni kweli bunge limesitisha kutoa mshahara na posho za Lissu tangu Januari?

Kagaigai: Malalamiko hayo hayajanifikia, mimi sijapata malalamiko hayo. Akakata simu.

Jana tarehe 13 Machi 2019 Lissu alitoa waraka aliousambaza akidai kuwa, bunge limezuia mshahara wake na posho za kibunge tangu mwezi Januari mwaka huu.

“Leo napenda kuthibitisha kwamba, uamuzi wa bunge kunifutia mshahara na posho zangu ulifanyika kabla hata ya Spika Ndugai (Job Ndugai) kuombwa na kutoa mwongozo huo.

“Ndio kusema kwamba bunge la Spika, Job Ndugai na Katibu wa Bunge, Stephen Kagaigai limezuia mshahara na posho za bunge tangu mwezi Januari mwaka huu,” imeeleza sehemu ya taarifa hiyo.

Lissu ambaye alikuwa Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) alikwenda Ubelgiji, tarehe 6 Januari mwaka jana, kufuatia kushambuliwa kwa risasi nje ya nyumba yake, Area D, mjini Dodoma na wanaoitwa na serikali, “watu wasiofahamika.”

Shambulio dhidi ya Lissu lilitokea tarehe 7 Septemba 2017, muda mfupi baada ya kushiriki mkutano wa Bunge wa asubuhi na kulihutubia Bunge.

error: Content is protected !!