Thursday , 28 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Bunge laishauri Serikali kuomba msaada IMF, WB vita ya corona
Habari za Siasa

Bunge laishauri Serikali kuomba msaada IMF, WB vita ya corona

Bunge la Tanzania
Spread the love

KAMATI ya Bunge ya Bajeti, imeishauri Serikali ya Tanzania kuliomba Shirika la Fedha Duniani (IMF), fedha kwa ajili ya kupambana na athari za janga la mlipuko wa virusi vya Corona (COVID-19). Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Wito huo umetolewa leo Ijumaa tarehe 15 Mei, 2020 bungeni jijini Dodoma na Mashimba Ndaki, Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti, wakati akiwasilisha maoni ya kamati hiyo, kuhusu bajeti ya Wizara ya Fedha na Mipango, katika mwaka wa fedha wa 2020/2021.

Ndaki  ameishauri Serikali kuomba msaada huo kupitia Mfuko wa Majanga wa IMF na Benki ya Dunia (WB), ili iweze kukabiliana na athari zinazotokana na janga la virusi vya Corona, ikiwemo mdororo wa kiuchumi katika sekta mbalimbali.

“Tumeshuhudia nchi jirani za Afrika Mashariki, Magharibi na Kusini mwa Afrika, zikipokea fedha kwa ajili ya kupambana na janga la Corona, pamoja na kusaidia sekta mbalimbali kupambana na mdoroo wa uchumi,” amesema Ndaki

“Kamati inaishauri Serikali kuangalia uwezekano wa kupata fedha hizo ili ziweze kusaidia kukabiliana na athari zinazotokana na janga la Covid-19. Uwezekano huo uangaliwe kwa kuzingatia faida na hasara za ahueni hiyo pamoja na kuzingatia Sheria ya Mikopo na Dhamana ya Serikali Sura ya 137.”

Wakati huo huo, kamati hiyo imeishauri wizara ya fedha na mipango kuandaa sera za kiuchumi, ili kusaidia kutatua matatizo ya kiuchumi yanayotokana na ugonjwa wa homa kali ya mapafu, inayosababishwa na virusi hivyo (Covid-19).

“Kamati inatoa ushauri kwa wizara ya fedha na mipango kuanza kufikiria namna ya kupanga sera zake za kiuchumi katika kipindi cha muda mfupi, wa kati na mrefu, ili kusaidia kutatua matatizo ya kiuchumi yatokanayo na Covid-19,” amesema Ndaki.

Ndaki amesema, Covid-19 inathiri kila Mtanzania na biashara kwa ujumla, hali inayoleta usumbufu wa utekelezaji wa shughuli za uchumi na msingi wa maoteo ya mapato, ulipaji na usimamizi wa kodi na mwenendo wa uchumi.

“Hivyo kuna umuhimu wa wizara hii kulazimika kufanya maamuzi muhimu ya sera kulingana na mazingira ya sasa kwa maendeleoi ya watu pamoja na ukusanyaji wa mapato,” amesema Ndaki.

Wakati huo huo, Ndaki amesema kamati ya bunge ya bajeti inaipongeza Serikali kupitia Benki Kuu ya Tanzania (BoT), kuchukua hatua za kudhibiti sekta ya fedha na upatikanaji wa huduma ya fedha katika shughuli za kiuchumi.

“Hatua za kushusha kiwango cha riba ya kukopeshana kati ya benki na mabenki kutoka asilimia 7 hadi 5 pamoja na kuongeza unafuu kwenye dhamana na hati fungani za serikali, ni matumaini ya kamati hatua hizi zitaenda kuwanufaisha na kuwasaidia wakopaji wa kawaida,” amesema Ndaki.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

Habari za SiasaTangulizi

CAG aibua madudu halmashauri 10, TANESCO na MSD

Spread the loveRIPOTI ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali...

error: Content is protected !!