December 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Bunge laibana Serikali mkataba wa KADCO

Bunge la Tanzania

Spread the love

 

BUNGE la Tanzania limeitaka Serikali kutoa ufafanuzi wa kwanini mkataba wa Kampuni ya Uendeshaji wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KADCO) umeendelea kuwepo licha ya Serikali kununua hisa zote za kampuni hiyo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Suala la uwepo wa mkataba huo liliibuliwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa mwaka unaoishia tarehe 30 Juni, 2021 na kufanyiwa uchambuzi na Kamati ya kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC).

Jana akiwasilisha taarifa ya Kamati kuhusu ripoti hiyo ya CAG, Makamu Mwenyekiti wa PAC, Japhet Hasunga, alisema uwepo wa mkataba huo unahitaji maelezo ya kina kutoka Serikalini.

Akitoa ufafanuzi wa jambo hilo leo Alhamis tarehe 3 Novemba, 2022, Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa alithibitisha kuwa ni kweli kampuni hiyo inamilikiwa na Serikali kwa asilimia 100 na watendaji wake wote ni watumishi wa Serikali.

Hata hivyo Spika Dk. Tulia Akson alihitaji ufafanuzi wa kwanini Mkataba ulioingiwa na wanahisa kabla ya kutwaliwa na Serikali umeendelea kuwepo hata baada ya kampuni hiyo kutwaliwa na Serikali kwa asilimia 100.

“Kimsingi KADCO iliyokuwepo awali haipo kisheria, sasa haya mazungumzo kuhusu mkataba yanatokana na nini, la pili kwanini hiyo KADCO baada ya kununuliwa haikurejeshwa TAA kama ilivyo kwa viwanja vingine…la tatu tunaona KADCO inailipa Serikali, hiyo KADCO inashikilia wapi hela halafu yenyewe ndiyo inailipa Serikali,” alihoji Spika Tulia.

Akijibu maswali hayo Mbarawa aliomba kutozunguzia zaidi kuhusu mkataba huo na kuahidi kulifanyia kazi na kutoa majibu ambapo Spika Tulia amempa hadi Jumamosi kuja na majibu hayo.

Kuhusu kurudishwa TAA, Mbarawa amesema tayari mpango huo upo na kuhusu akaunti, amesema KADCO ina akaunti Benki Kuu kama ilivyo kwa taasisi zimngine za Serikali na inapofanya malipo hutoka kwenye akaunti hiyo kwenda Serikalini.

error: Content is protected !!