Friday , 3 February 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Bunge lahofia mwenendo upatikanaji fedha za bajeti
Habari za Siasa

Bunge lahofia mwenendo upatikanaji fedha za bajeti

Waziri Mkuu akihutubia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Spread the love

 

KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii, imesema kusuasua kwa mwenendo wa utoaji fedha za bajeti kutoka serikalini, unakwamisha kasi ya utekelezaji miradi ya maendeleo. Anaripoti Nasra Bakari, DMC…(endelea).

Kwa mujibu wa taarifa ya kamati hiyo, kuhusu utekelezaji wa bajeti ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi 2020/21, hadi Machi 2021, wizara hiyo ilipokea asilimia 33.9, ya fedha zilizoidhinishwa katika bajeti hiyo.

Taarifa hiyo iliyowasilishwa leo tarehe 26 Mei 2021, bungeni jijini Dodoma, imesema ikiwa imesalia takribani mwezi mmoja, kwa bajeti hiyo kuisha muda wake, wizara imepokea Sh. 44.64 bilioni, kati ya Sh. 131.49 bilioni, iliyoidhinishwa na Bunge mwaka jana.

“Wizara iliidhinishiwa na Bunge bajeti ya Sh. 129.57 bilioni na badae kupata nyongeza ya Sh. 1.91 bilioni na kufanya bajeti ya wizara kuongezeka, kuwa na jumla ya Sh. 131.49 bilioni.

Hadi kufikia Machi 2021, Wizara ilipokea jumla ya Sh. 44.64 bilioni, ikiwa ni sawa na asilimia 33.9 ya bajeti iliyoidhinishwa kwa Mwaka wa Fedha 2020/2021,” imesema taarifa ya kamati hiyo.

Taarifa hiyo imesema katika bajeti hiyo, wizara ilipangiwa Sh. 47.40 bilioni kwa ajili ya matumizi ya kawaida, ambapo hadi Machi 2021, ilipokea Sh. 39.26 bilioni, sawa na asilimia 76.65.

Wakati bajeti ya fedha za miradi ya maendeleo ilipangiwa Sh. 84.08 bilioni, lakini hadi kufikia kipindi hicho, ilipatiwa Sh. 5.37 bilioni sawa na asilimia 30.2.

“Kati ya fedha zilizopokelewa, Sh. 39.26 bilioni ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida sawa na asilimia 76.65, ya bajeti iliyotengwa kwa shughuli hiyo na Sh. 5.37 bilioni sawa na asilimia 30.2, zilikuwa ni kwa ajili ya miradi ya maendeleo,” imesema taarifa hiyo.

Taarifa hiyo imesema, Kamati ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi iliidhinishiwa Sh. 4.66 bilioni, kwa ajili ya matumizi ya kawaida, lakini hadi kufikia tarehe 15 Machi 2021, ilipokea Sh. 2.01 bilioni, sawa na asilimia 43 ya fedha iliyoidhinishwa katika bajeti hiyo.

Job Ndugai Spika wa Bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania

Kamati hiyo imesema tume hiyo iliidhinishiwa Sh. 1.50 bilioni, kwa ajili ya utekelezaji miradi ya maendeleo. Lakini hadi tarehe 15 Machi 2021, haikupewa fedha hizo.

“Kamati ina maoni kuwa, mwenendo huu wa upatikanaji wa fedha, unakwamisha kasi na viwango vya utekelezaji wa miradi ya maendeleo. Upungufu huu wa kibajeti unaifanya Tume ishindwe kutekeleza majukumu yake ya msingi,” imesema taarifa ya kamati hiyo na kuongeza:

“Kwa mfano, kuhuisha Mpango wa Taifa wa Matumizi ya Ardhi wa mwaka 2013 – 2033. Vilevile, kuandaa Mipango ya Kanda ya Matumizi ya Ardhi, Mipango ya Ardhi ya Wilaya na kuratibu uandaaji wa mipango ya ardhi ya vijiji katika vijiji vyote nchini.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Vijana ACT-Wazalendo Dar wampa tano Rais Samia

Spread the love  NGOME ya Vijana ya Chama cha ACT-Wazalendo, kimempongeza Rais...

Habari za Siasa

ACT-Wazalendo yaiangukia Serikali kunusuru wananchi Liwale, Nachingwea

Spread the love  CHAMA cha ACT-Wazalendo, kimeitaka Serikali kuchukua hatua za haraka...

Habari za SiasaTangulizi

Vigogo wanaokwamisha mradi Liganga na Mchuchuma kitanzani

Spread the love  NAIBU Spika wa Bunge, Mussa Zungu, watu wanaokwamisha utekelezaji...

Habari za Siasa

Gridi ya Taifa kufumuliwa kukabiliana na katizo la mgao wa umeme

Spread the love  WAZIRI wa Nishati, Januari Makamba, amesema Serikali ina mpango...

error: Content is protected !!