Sunday , 25 February 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Bunge lafanya vioja, ripoti ya Lissu yayeyuka
Habari za Siasa

Bunge lafanya vioja, ripoti ya Lissu yayeyuka

Adadi Rajabu, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ulinzi, Usalama na Mambo ya Nje
Spread the love

TAARIFA iliyotarajiwa kuwasilishwa bungeni leo na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ulinzi, Usalama na Mambo ya Nje, Adadi Rajabu kuhusu kushambuliwa kwa Tundu Lissu, Mbunge wa Singida Mashariki imeota mbawa, anaandika Dany Tibason.

Taarifa hiyo ambayo ilikuwa ikisubiriwa kwa hamu na wabunge pamoja na wananchi imeshindwa kuwasilishwa bungeni kutokana na mwenyekiti wa kamati hiyo kudai kuwa muda wa kamati hiyo kufanya kazi kwa ufasaha haukutosha.

Rajabu ambaye ni mbunge wa Mheza (CCM), ametoa kauli hiyo leo bungeni baada ya kupewa muda wa kuelezea Bunge kama angewasilisha ripoti hiyo kama alivyokuwa ameagizwa na Spika.

Spika Job Ndugai aliunda kamati hiyo kuchunguza shambulio la kupigwa risasi mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (Chadema).

Kamati hiyo na Spika kupokea mwongozo wa Mbunge wa Nzega Mjini Husein Bashe (CCM) ambaye alitaka kufanyika uchunguzi wa Bunge ili kubaini waliomshambulia Lissu.

Naibu Spika, Tulia Ackson alitoa nafasi kwa mwenyekiti wa kamati hiyo ili atoe maelezo kama angetoa ripoti bungeni au la kwani haikuwemo katika ratiba za shughuli za Bunge.

“Kama mnavyojua waheshimiwa wabunge Spika aliombwa mwongozo na mbunge wa Nzega Mjini Mheshimiwa Bashe, akitaka kuchunguza masuala ya uasalama wa nchi na wabunge,” amesema

“Lakini tunaona katika orodha yetu ya shughuli za Bunge sioni kama taarifa hiyo itawasilishwa na kabla sijasema lolote naomba basi nimpatie mwenyekiti wa kamati ili aweze kutuelezea kama atawasilisha taarifa hiyo au la” amesema

Baada ya kupatiwa mud, Adadi Rajabu amesema kamati imeshindwa kukamilisha taarifa hiyo kutokana na kupewa muda mfupi kulingana na unyeti wa kazi husika.

“Tulitakiwa kuwasilisha taarifa kama ilivyokuwa imeelezwa na Spika, lakini tumeshindwa kutokana na kuwa muda ulikuwa mfupi, lakini tunaomba ruhusa Spika atuongezee muda ili tuweze kuifanyia kazi na kutoa taarifa kwa wabunge” amesema

Baada ya maelezo hayo ya Naibu Spika alimtaka mwenyekiti wa kamati kumwandikia Spika barua ili ombi hilo liweze kusomwa kwa wabunge.

“Kutokana na ombi lako unatakiwa kumwandikia barua haraka sana Spika ili aweze kuwatangazia wabunge kabla hawajatawanyika kwenda majimbani kwao” amesema

Akiomba mwongozo Bashe alisema kutokana na kuwepo kwa matukio mbalimbali ya utekaji, unyanyasaji na mauaji bila kuwepo na taarifa rasmi kutoka katika vyombo ya ulinzi na usalama kumewafanya wabunge wengi kuwa na taruki huku wakihofia kupoteza maisha yao kwa kukosa ulinzi wa uhakika.

Bashe alitoa hoja ya kupotea kwa Ben Saanane, kutekwa kwa Roma Mkatoloki, kutishiwa Nape Nnauye na bastora huku wakihoji ni kwanini hakuna taarifa sahihi kutoka katika vyombo vya ulinzi na usalama.

Baada ya kumalizika kwa kipindi cha maswali na majibu baadhi ya wabunge wengi walisimama na kuomba mwongozo wa Spika.

Walioomba mwangozi siku hiyo mbunge wa Nzega mjini Husein Bashe,(CCM), mbunge wa Ukonga, Mwita Waitara (Chadema), Mbunge wa Ulanga Goodruck Mlinga (CCM) pamoja na mbunge wa Arumeru Magharibi, Joshua Nasari

Spika alimruhusu Bashe kuwa wa kwanza kuomba mwongozo ambapo alisema kuwa anaomba mwongozo kwa jambo la dharula kwa kanuni 47, kanuni ya kwanza na ya pili na kueleza kuwa iwapo Spika ataridhia yeye atatumia kanuni ya nne kuruhusu jambo hilo na iwapo wabunge wataona inafaa aliwaomba wamuunge mkono.

Naye mbunge wa Ukonga Mwita Waitara alipopewa nafasi kutoa mwongozo wake alisema alikuwa nataka kutoa hoja ambayo tayari imeisha tolewa na Bashe.

Baada ya Bashe kutoa hoja hiyo wabunge wote wa upinzani walisimama kuunga mkono hoja huku wabunge wa CCM wakionekana kusimama kwa mashaka.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Samia atoa pole ajali iliyoua 25, kujeruhi 21 Arusha

Spread the loveRais Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za rambirambi kwa Mkuu...

Habari za SiasaTangulizi

Dk. Biteko afuta likizo watumishi Tanesco, bosi Morogoro yamkuta

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dk. Doto...

Habari za Siasa

Mbarala ajitosa kumrithi Zitto, aahidi kuipa ushindi ACT-Wazalendo uchaguzi mkuu

Spread the loveKATIBU wa Idara ya Haki za Binadamu na Makundi Maalum...

Habari za Siasa

Dorothy Semu ajitosa kumrithi Zitto ACT-Wazalendo

Spread the loveMAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha ACT-Wazalendo, anayemaliza muda wake, Dorothy...

error: Content is protected !!