Friday , 3 February 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Bunge laahirishwa, maswali 1,468 yaulizwa
Habari za Siasa

Bunge laahirishwa, maswali 1,468 yaulizwa

Kassim Majaliwa, Waziri Mkuu wa Tanzania
Spread the love

 

KASIM Majaliwa, Waziri Mkuu wa Tanzania ameahirisha shughuli za Bunge la 12 la Tanzania leo Jumatano, tarehe 30 Juni 2021, jijini Dodoma mpaka tarehe 31 Agosti 2021 litakapokutana tena. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Akizungumza wakati wa kuahirisha bunge hilo, Waziri Majaliwa amesema serikali itafanyia kazi ushauri uliotolewa katika vikao vya mkutano huo wa tatu wa bunge hilo.

“Leo Bunge limehitimisha shughuli zote zilizopangwa, katika mkutano wa tatu wa Bunge la 12. Serikali kwa upande wake itazingatia ushauri wote uliotolewa na Bunge, kwa lengo la kuboresha utekelezaji wa mipango na bajeti kwa manufaa ya Watanzania,” amesema Waziri Majaliwa.

Akielezea shughuli zilizofanyika katika mkutano huo, Waziri Majaliwa amesema, takribani maswali 528 ya msingi na mengine 1,468 ya nyongeza, yaliulizwa na wabunge na kujibiwa na serikali.

Huku maswali ya papo kwa papo yaliyoulizwa na wabunge kwa Waziri Mkuu, yakiwa 21.

Pia, Waziri Majaliwa amesema mkutano huo, wabunge walipitisha maazimio mawili ya Bunge, ambayo ni mhimili huo kuutambua na kuuenzi mchango wa aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano, Hayati John Magufuli.

Na azimio la kumpongeza Samia Suluhu Hassan, kuwa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Rais Samia aliingia madarakani tarehe 19 Machi 2021, baada ya Rais Magufuli kufariki dunia tarehe 17 Machi mwaka huu, katika Hospitali ya Mzena mkoani Dar es Salaam, alikokuwa anapatiwa matibabu ya ugonjwa wa moyo.

Waziri Mkuu akihutubia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mbali na bunge hilo kupitisha maazimio hayo, lilijaidli na kupitisha miswada ya sheria mitatu, ikiwemo Muswada wa Sheria ya Fedha za Matumizi wa Mwaka 2021.

Pia muswada wa Sheria ya Fedha wa Mwaka 2021 na Muswada wa Sheria ya Mabadiliko ya Sheria mbalimbali Na. 3 wa mwaka 2021.

“Aidha, Muswada wa Sheria ya Mabadiliko ya Sheria mbalimbali Na. 4 wa 2021 na Muswada wa Sheria ya Mabadiliko ya Sheria ya Usalama Barabarani wa 2021, imesomwa kwa mara ya kwanza,” amesema Waziri Majaliwa.

Waziri Majaliwa amesema, bunge hilo lilijadili na kuupitisha Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa kwa kipindi cha miaka mitano kuanzia 2021/22 hadi 2025/2026.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Kamati ya Bunge yaitaka Serikali kuchunguza dawa za asili

Spread the love  KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo...

Habari za Siasa

Kada NCCR-Mageuzi aliyepotea aokotwa porini akiwa taabani, hajitambua

Spread the love  MWENYEKITI wa Jumuiya ya Vijana ya Chama cha NCCR-Mageuzi,...

Habari za Siasa

ACT Wazalendo yataka Jaji Mkuu, Jaji Biswalo wajiuzulu kupisha uchunguzi fedha za Plea Bargaining

Spread the love  CHAMA cha ACT-Wazalendo, kimemtaka Jaji wa Mkuu wa Tanzania,...

Habari za Siasa

Kigogo ACT-Wazalendo: Vyama vya upinzani vilikosea kumpokea Membe, Lowassa

Spread the love  KATIBU Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, Ado Shaibu, amesema...

error: Content is protected !!