Monday , 22 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Bunge laagiza Mdude wa Chadema atafutwe
Habari za Siasa

Bunge laagiza Mdude wa Chadema atafutwe

Mdude Nyagari
Spread the love

SAKATA la kada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Mdude Nyagawa limetua bungeni ambapo sasa, Bunge limetaka maelezo kujua alipo. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Bunge limeiagiza serikali kufuatilia taarifa za kada huyo baada ya kutekwa na watu wasiojulikana na kisha kutoweka naye. Habari za kutekwa kwa Dude zimeendelea kusambaa katika mitandao ya kijamii zikihoji alipo Mdude.

Wito huo umetolewa leo tarehe 6 Mei 2019 bungeni jijini Dodoma na Mwenyekiti wa Bunge, Andrew Chenge baada ya Mbunge wa Iringa Mjini, Peter Msigwa kutoa hoja ya kuahirisha kikao kwa ajili ya kujadili sakata hilo.

Awali Chenge aliitaka serikali itoe maelezo ili wananchi wajue hali ilivyo, kwa kuwa suala hilo linahusu uhai wa binadamu.

Akifafanua kuhusu sakata hilo, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni amesema, Jeshi la Polisi limeanza kufanya uchunguzi wa tukio la kupotea kwa Mdude tangu tarehe 5 Mei 2019.

Mhandisi Masauni amewataka Watanzania kutoa ushirikiano kwa vyombo vya dola utakaowezesha kupatikana kwa Mdude.

Mdude anadaiwa kutekwa na watu wasiojulikana tangu tarehe 4 Mei 2019, akiwa ofisini kwake Mbozi Mkoa wa Songwe.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Rais Samia aridhishwa utendaji mabalozi, awapa neno

Spread the loveRais wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan amewapongeza mabalozi  wanaowakilisha ...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

NMB yadhamini Mkutano Mkuu ALAT, kufunguliwa na Samia

Spread the loveBENKI ya NMB, imekabidhi hundi yenye thamani ya Sh. 120...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mipango na uwekezaji kutumia bilioni 121.3, mradi wa Bagamoyo wapewa kipaumbele

Spread the loveWIZARA ya Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, imeliomba Bunge...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mbunge ataka kasi uzalishaji walimu ipunguzwe akidai hakuna ajira

Spread the loveMBUNGE wa Mlalo (CCM), Rashid Shangazi, ameishauri Serikali ipunguze kasi...

error: Content is protected !!