January 17, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Bunge la Tanzania kusukwa upya

Job Ndugai, aliyekuwa Spika wa Bunge Tanzania

Spread the love

 

BUNGE la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, linatarajiwa kusukwa upya, baada ya kung’oka mamlakani kwa Spika wake, Job Ndugai. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es salaam … (endelea).

Spika Ndugai alitangaza kujiuzulu jana mchana Alhamisi, tarehe 6 Januari 2022, baada ya shinikizo kutoka ndani ya chama chake – Chama Cha Mapinduzi (CCM) – hasa yakikolezwa na wabunge, waliokuwa mbioni kupeleka hoja binafsi ya kumwondoa bungeni.

Katika taarifa yake kwa umma, Ndugai alisema, “naomba kutoa taarifa kwa umma, kuwa leo Januari 6, nimeandika barua kwenda kwa Katibu wa CCM, kujiuzulu nafasi ya Spika wa Bunge, uamuzi huu ni binafsi na hiyari na nimeufanya kwa kuzingatia na kujali maslahi mapana zaidi ya Taifa langu, Serikali na CCM.”

Aliongeza: “Nakala ya barua yangu ya kujiuzulu, nimewasilisha kwa Katibu wa Bunge, kwa ajili ya hatua stahiki kwa mujibu wa Katiba ya nchi na sheria nyingine husika, ili kuwezesha mchakato wa kumpata Spika mwingine uweze kuanza.”

Miongoni mwa wanaotajwa kumrithi Ndugai, ni pamoja na Mbunge wa Ilala, Mussa Azzan Zungu; wa Kibakwe mkoani Dodoma, George Simbachawene, aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Brazil, Dk Emmanuel Nchimbi na Dk. Tulia Ackson ambaye ni naibu spika wa sasa.

Mabadiliko gani yanakwenda kufanyika ndani ya Bunge, soma gazeti la Raia Mwema, la leo Ijumaa tarehe 7 Januari 2022, limeyachambua kutoka vyanzo vya ndani.

error: Content is protected !!