April 15, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Bunge la Ndugai laamua kumtenga Prof. Assad

Prof. Mussa Assad alipohojiwa na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maadili, Haki na Madaraka ya Bunge

Spread the love

BUNGE la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, limeazimia kutofanya kazi na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad, kwa madai ya kwenda kinyume na kifungu cha 26 cha Sheria ya Kinga ya Madaraka na Haki za Bunge. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Bunge limepitisha azimio hilo leo tarehe 2 Aprili 2019 mbele ya Naibu Spika, Dk. Tulia Ackson jijini Dodoma baada ya Kamati ya Maadili na Madaraka ya Bunge kuwasilisha taarifa yake ya kumhoji Prof. Assad.

Prof. Assad alihojiwa baada ya Spika wa Bunge, Job Ndugai kupelekea shauri dhidi yake katika kamati hiyo, akimshitaki kwa madai ya kutoa kauli za kudhalilisha bunge, wakati akifanya mahojiano na kituo cha Redio cha Umoja wa Mataifa nchini Marekani.

Emmanuel Mwakasaka, Mweyekiti wa Kamati ya Maadili na Madaraka ya Bunge wakati akisoma ripoti ya kamati hiyo mbele ya bunge, amesema katika uchunguzi wake kuhusu shauri la Prof. Assad, ulibaini kwamba alikiuka masharti ya kifungu cha 26 E cha Sheria ya Kinga, Haki na Madaraka ya Bunge kwa kutamka maneno ya kulidhalilisha bunge.

Mwakasaka amesema, Prof. Assad wakati akihojiwa na kamati hiyo, hakujutia kosa lake.

 “Kwa kuwa alionesha dharau kwa kamati wakati wa mahojiano na hakujutia kutenda kosa alilofanya la kudharau na kudhalilisha bunge, na aliendelea kusititza kuwa, ataendelea kutumia maneno yanayolalamikiwa kudhalilisha Bunge,” amesema Mwakasaka na kuongeza;

 “Kwa kuwa kamati ilimtia hatiani Prof. Assad kwa kosa la kudharau na kudhalilisha bunge kinyume cha kifungu 26 E cha sheria ya kinga ya madaraka na haki za bunge sura 296, kanuni ya 54 fasihi ya 123 kanuni za kudumu ya bunge toleo 2016, inalipa bunge mamalaka ya kupokea na kujadili mapendekezo ya kamati hii na kisha kufanya uamuzi kwa njia ya maazimio.”

“Bunge linaazimia kwamba, haliko tayari kufanya kazi na Prof. Assad…, bunge haliko tayari kushirikiana naye kwa sababu, kutokana na majukumu yake ya udhibiti na ukaguzi wa hesabu serikali kutakiwa kufanya kazi zake na bunge ambalo tayari ameonesha kulidharau na kulidharirisha, kwa hiyo bunge linaazimia haliko tayari kufanya kazi na CAG.”

error: Content is protected !!